Title : Tetesi za usajili: Manchester United kumlipa Griezmann paundi 220,000 kwa wiki, Mousa Dembele kutua EPL, Ighalo kwenda Uchina, Manchester United kumrudisha Evra
link : Tetesi za usajili: Manchester United kumlipa Griezmann paundi 220,000 kwa wiki, Mousa Dembele kutua EPL, Ighalo kwenda Uchina, Manchester United kumrudisha Evra
Tetesi za usajili: Manchester United kumlipa Griezmann paundi 220,000 kwa wiki, Mousa Dembele kutua EPL, Ighalo kwenda Uchina, Manchester United kumrudisha Evra
FOWADI wa Atletico Madrid Antoine Griezmann, 25, amepewa ofa ya paundi 220,000 kwa wiki na Manchester United - kiwango sawa na anacholipwa mfaransa-mwenza Paul Pogba. (Sun)
United inaandaa ofa ya paundi 32.5m kuinasa saini ya mlinzi wa AS Roma Kostas Manolas, 25, baada ya dili la kumsajili Victor Lindelof, 22, kutoka Benfica kugonga mwamba. (Sun)
Mlinzi wa kushoto wa Juventus Patrice Evra, 35, amefanya mazungumzo na West Ham na klabu yake ya zamani Manchester United kuhusu uhamisho Januari. (Calciomercato.com)
West Ham imemuongeza mshambuliaji wa Celtic Moussa Dembele, 20, katika orodha ya wachezaji wanaowahitaji na wako tayari kutumia paundi 20m kuinasa saini yake. (Goal)
Hata hivyo, the Hammers watalazimika kuongeza ofa hadi paundi 30m kumnasa Mfaransa huto. (Daily Mail)
Chelsea ingali katika mazungumzo na Atalanta juu ya uwezekano wa kumsajili Franck Kessie, 20, lakini vinara hao wa Premier League italazimika kusubiri hadi majira ya joto. (Guardian)
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anavutiwa na mshambuliaji wa Torino Andrea Belotti, 23, lakini hawezi kulipa paundi 50m kumsajili. (Sun)
Mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo, 27, anataka kuondoka Watford, ambapo Hornets wakitegemea fedha nyingi kutoka klabu inayocheza Chinese Super League ya Shanghai Shenhua. (Mirror)
Kutoka na mustakabali wa James Rodriguez, 25, kuwa katika uwiano sawa katika klabu ya Real Madrid, mwandishi wa Italia Mina Rzouki anaamini Manchester United wanaweza kuinasa saini yake. (BBC Radio 5 live)
Mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28, amesema anaweza kufungiwa hadi "mechi nne au tano" kama akitoa mawazo yake ya kweli kuhusu waamuzi wa Uingereza. (Onda Cero)
Bayer Leverkusen haijapokea ofa kutoka Chelsea kwa ajili ya mshambuliaji Javier Hernandez, 28, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo. (Talksport)
Liverpool inajiandaa kumuuza mlinzi Tiago Ilori, 23, katika klabu ya Reading kwa paundi 3.75m. (Liverpool Echo)
Fowadi Bojan, 26, yupo tayari kuondoka Stoke City kwa ajili ya kupata namba ya kudumu. (Stoke Sentinel)
Boss mpya wa Crystal Palace Sam Allardyce anaweza kumfanya mshambuliaji wa Motherwell Louis Moult, 24, usajili wake wa kwanza, klabu hiyo ikiandaa ofa ya paundi 500,000. (Talksport)
Kazi ya Slaven Bilic katika klabu ya West Ham haiko salama kama watu wafikiriavyo, kwa mujibu wa mwandishi Tony Evans. (BBC Radio 5 live)
Aston Villa imeambiwa watalazimika kulipa paundi 10m kumsajili Jordan Rhodes, 26, kutoka Middlesbrough. (Mirror)
Meneja mpya wa Hull Marco Silva ametoa ahadi kuwa anaweza kufanya nyongeza ya wachezaji muhimu Januari. (Daily Mail)
Birmingham City imetoa ombi la kumchukua kiungo wa West Brom Craig Gardner, 30, kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu. (Birmingham Mail)
Thus articles Tetesi za usajili: Manchester United kumlipa Griezmann paundi 220,000 kwa wiki, Mousa Dembele kutua EPL, Ighalo kwenda Uchina, Manchester United kumrudisha Evra
that is all articles Tetesi za usajili: Manchester United kumlipa Griezmann paundi 220,000 kwa wiki, Mousa Dembele kutua EPL, Ighalo kwenda Uchina, Manchester United kumrudisha Evra This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article Tetesi za usajili: Manchester United kumlipa Griezmann paundi 220,000 kwa wiki, Mousa Dembele kutua EPL, Ighalo kwenda Uchina, Manchester United kumrudisha Evra the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2017/01/tetesi-za-usajili-manchester-united_6.html
0 Response to "Tetesi za usajili: Manchester United kumlipa Griezmann paundi 220,000 kwa wiki, Mousa Dembele kutua EPL, Ighalo kwenda Uchina, Manchester United kumrudisha Evra"
Post a Comment