UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: FC Basel v Arsenal: Wenger kumpumzisha Alexis Sanchez na kumpa nafasi Perez?

UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: FC Basel v Arsenal: Wenger kumpumzisha Alexis Sanchez na kumpa nafasi Perez? - Hallo friend ALL NEW, In the article you read this time with the title UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: FC Basel v Arsenal: Wenger kumpumzisha Alexis Sanchez na kumpa nafasi Perez?, we have prepared well for this article you read and download the information therein. hopefully fill posts Article Culinary, Article Culture, Article Economy, Article Politics, Article Sports, Article The latest, Article Updated, we write can understand. Well, happy reading.

Title : UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: FC Basel v Arsenal: Wenger kumpumzisha Alexis Sanchez na kumpa nafasi Perez?
link : UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: FC Basel v Arsenal: Wenger kumpumzisha Alexis Sanchez na kumpa nafasi Perez?

Read also


UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: FC Basel v Arsenal: Wenger kumpumzisha Alexis Sanchez na kumpa nafasi Perez?

Arsenal inaweza kumpumzisha fowadi Alexis Sanchez kwenye mchezo wa mwisho wa Champions League hatua ya makundi Kundi A ugenini dhidi ya Basel.
Tayari the Gunners imeshafuzu hatua ya mtoano na itamaliza nafasi ya pili kwenye kundi lake kwa matokeo yoyote kama Paris St-Germain itaifumua Ludogorets Razgrad.
Kama fowadi wa kimataifa wa Chile Sanchez ataachwa, itakuwa nafasi ya mshambuliaji wa Uhispania Lucas Perez.
Kiungo Granit Xhaka anarejea kwenye klabu yake ya zamani Basel, ambayo inapambana na Ludogorets kutafuata nafasi kwenye Europa League.
Miamba hiyo ya soka la Uswisi inawaombea dua mbaya Ludogorets ya Bulgaria ichapwe na mabingwa wa Ufaransa PSG na wenyewe angalau wapate pointi moja.
Arsenal imekuwa ikiondolewa hatua ya 16 kwenye misimu sita iliyopita na imemaliza nafasi ya pili hatua ya makundi kwenye misimu mitano iliyopita.
Hata hivyo, msimu huu unaweza ukafuta historia ya kumaliza nafasi ya pili ambao husababisha kuwa na mpinzani mgumu kwenye mchezo wa mtoano.
Kuelekea siku ya mwisho, timu zote za Porto, Real Madrid, Bayern Munich na Benfica zipo katika nafasi ya pili kwenye makundi yao.
Boss wa Gunners Arsene Wenger alisema hivi karibuni kuwa amekuwa akiachwa na hasira timu yake inapokutana na mpinzani mgumu hatua ya 16 lakini, katika tukio ambalo Arsenal itamaliza nafasi ya pili tena, 2017 utakuwa tofauti.
"Inaonekana hata kama ukimaliza nafasi ya kwanza au ya pili," alisema Wenger Jumatatu.
"Faida ya kumaliza nafasi ya kwanza ni kuwa unacheza mchezo wa pili nyumbani, na uwezekano wa dakika 30 za nyongeza nyumbani.
"Tutaona. PSG wataifunga Ludogorets nyumbani na kushika uongozi wa kundi, lakini tutaangalia ubao wa matokeo wakati wa mapumziko na kuona tunakwenda wapi."

Dondoo muhimu kuzifahamu

  • Arsenal imeshinda mechi zote tano zilizopita dhidi ya timu za Uswisi.
  • Basel imeshinda mechi tatu zilizopita za Champions League ilizocheza nyumbani dhidi ya timu za Uingereza.
  • Basel imepoteza mara mbili kati ya michezo minane ya Champions League iliyocheza nyumbani, vichapo hivyo ilikuwa dhidi ya Real Madrid na PSG.
  • Arsenal haijapoteza mchezo kwenye kampeni za Champions League hatua ya makundi tangu msimu 2005-06.
  • Hakuna mchezo kati ya michezo 40 ya Arsenal iliyocheza ugenini kwenye Champions League uliomalizika kwa sare ya bila kufungana. Sare yao 0-0 ya hivi karibuni ilikuwa dhidi ya Slavia Prague mwezi Novemba 2007.

Mechi nyingine Jumanne; Paris St-Germain watakuwa nyumbani kuwakaribisha Ludogorets Razgrad huku Napoli wakiwa wageni wa Benfica na Besiktas wakialikwa na Dynamo Kiev.

Barcelona watakuwa Camp Nou kuwakaribisha B Gladbach huku Manchester City wakiwa wenyeji wa Celtic na Bayern Munich wakiwa nyumbani dhidi ya Atletico Madrid na PSV Eindhoven wakitifuatana na FC Rostov.



Thus articles UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: FC Basel v Arsenal: Wenger kumpumzisha Alexis Sanchez na kumpa nafasi Perez?

that is all articles UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: FC Basel v Arsenal: Wenger kumpumzisha Alexis Sanchez na kumpa nafasi Perez? This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.

You are now reading the article UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: FC Basel v Arsenal: Wenger kumpumzisha Alexis Sanchez na kumpa nafasi Perez? the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/uefa-8-viwanjani-leo-uefa-match-preview.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: FC Basel v Arsenal: Wenger kumpumzisha Alexis Sanchez na kumpa nafasi Perez?"

Post a Comment