Title : EPL: Chelsea 2-1 Tottenham: Chelsea yatakata EPL
link : EPL: Chelsea 2-1 Tottenham: Chelsea yatakata EPL
EPL: Chelsea 2-1 Tottenham: Chelsea yatakata EPL
Chelsea ilirejea kileleni mwa msimamo wa Premier League baada ya kutoka nyuma na kuichapa Tottenham mabao 2-1 kwenye mchezo wa Premier League uliopigwa Stamford Bridge ikiwa ni kichapo cha kwanza kwa Tottenham kwenye Premier League msimu huu.
Spurs ilijaribu kufuta machungu ya kutolewa kwenye Champions League katikati ya wiki baada ya bao la Christian Eriksen dakika ya 11 kuwaweka mbele.
Vijana wa Mauricio Pochettino walionekana kuutawala mchezo mpaka dekunde chache kabla ya mapumziko ambapo Pedro aliisawazishia Chelsea.
Na rekodi mbaya ya Spurs kwenye dimba la Stamford Bridge iliendelea na kufikia mechi 30 bila ushindi - tangu Februari 1990 - baada ya Victor Moses kufunga bao la pili kwa Chelsea dakika sita baada ya kuanza kipindi cha pili.
Mlinda mlango wa Spurs Hugo Lloris na Jan Vertonghen wote waliugusa mpira uliopigwa na Moses lakini hata hivyo ulikwenda moja kwa moja wavuni huku Chelsea ikirekodi ushindi wa saba mfululizo kwenye ligi.
Kifuatacho?
Chelsea itasafiri kuifuata Manchester City Jumamosi ijayo kwa mchezo baina ya vinara na timu ya nafasi ya pili kwenye Premier League. Tottenham watakuwa nyumbani dhidi ya Swansea siku hiyo.
Thus articles EPL: Chelsea 2-1 Tottenham: Chelsea yatakata EPL
that is all articles EPL: Chelsea 2-1 Tottenham: Chelsea yatakata EPL This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article EPL: Chelsea 2-1 Tottenham: Chelsea yatakata EPL the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/11/epl-chelsea-2-1-tottenham-chelsea.html
0 Response to "EPL: Chelsea 2-1 Tottenham: Chelsea yatakata EPL"
Post a Comment