Title : EPL: Premier League round-up: Manchester City, Liverpool na Swansea zaishinda, Pardew njia panda na Leicester hali si hali
link : EPL: Premier League round-up: Manchester City, Liverpool na Swansea zaishinda, Pardew njia panda na Leicester hali si hali
EPL: Premier League round-up: Manchester City, Liverpool na Swansea zaishinda, Pardew njia panda na Leicester hali si hali
BAADA ya Manchester City kukimbilia kileleni mapema baada ya kuichapa Burnley mabao 2-1, lakini hata hivyo hawakukaa sana baada ya Liverpool kuwapora nafasi hiyo ambayo nayo iliirejesha kwa Chelsea iliyoichapa Tottenham mabao 2-1.
Haya ni matokeo ya mechi zote za Premier League:
Liverpool 2 - 0 Sunderland
Liverpool iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Sunderland kwenye mchezo uliokuwa mgumu kwao katika dimba la Anfield.
Vijana wa Jurgen Klopp walikuwa na hali ngumu sana wakipambana na vijana wa David Moyes wakionekana kama wangalimaliza kwa sare ya pili mfululizo.
Lakini bao la Divock Origi dakika 15 kabla ya fililmbi ya mwisho ikavunja kufuli na James Milner akafunga bao la pili kwa mkwaju wa penalti.
Leicester City 2 - 2 Middlesbrough
Leicester City iliambulia sare ya dakika za lala salama kwenye mchezo uliopigwa King Power dhidi ya Middlesbrough.
Alvaro Negredo alifunga bao lake la pili msimu huu baada ya kuipa Boro uongozi kufuatia kazi nzuri ya Gaston Ramirez.
Leicester walipewa nafasi ya kusawazisha baada ya Callum Chambers kuushika mpira katika box. Riyad Mahrez akafunga kwa penalti.
Negredo alionekana kuipa timu ngeni pointi tatu muhimu akiyatumia vema makosa ya safu ya ulinzi wa Foxes akimalizia kazi nzuri ya Adam Forshaw kabla ya kumtungua Ron-Robert Zieler.
Lakini Islam Slimani alifunga bao la kusawazisha kwa penalti dakika za lala salama baada ya Wes Morgan kuangushwa kwenye box.
Swansea City 5 - 4 Crystal Palace
Bob Bradley alipata ushindi wa kwa wa ligi tangu kuchukua mikoba ya kuifundisha Swansea timu hiyo ikiichapa Crystal Palace mabao 5-4 katika dimba la Liberty.
Wilfried Zaha alifungua ukurasa wa mabao kwa Eagles baada ya mpira uligongwa na Christian Benteke kumkuta mfungaji.
Lakini Swansea ikasawazisha shukrani kwa Gylfi Sigurdsson aliyefunga kwa free-kick dakika 10 kabla ya mapumziko.
Leroy Fer akafunga mabao mawili ya haraka kuipa timu mwenyeji uongozi wa mabao 3-1 kabla ya Crystal Palace kutoka nyuma na kufanya matokeo kuwa mabao 4-3, kwa mabao ya James Tomkins, bao la kujifunga kutoka kwa Jack Cork na shuti la Benteke.
Lakini Swansea wakafunga mabao mawili katika muda wa nyongeza kupitia kwa Fernando Llorente na kuongeza presha kwa meneja wa Palace Alan Pardew.
Hull na West Brom zilitoka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo uliopigwa KCOM Stadium huku mweneji akitoka nyuma kupata pointi moja.
The Baggies waliongoza baada ya Gareth McAuley kufunga kwa kichwa kutokana na kazi nzuri ya Matt Phillips.
Lakini Michael Dawson ilisawazisha kipindi cha pili baada ya Robert Snodgrass kufunga kwa free-kick.
Thus articles EPL: Premier League round-up: Manchester City, Liverpool na Swansea zaishinda, Pardew njia panda na Leicester hali si hali
that is all articles EPL: Premier League round-up: Manchester City, Liverpool na Swansea zaishinda, Pardew njia panda na Leicester hali si hali This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article EPL: Premier League round-up: Manchester City, Liverpool na Swansea zaishinda, Pardew njia panda na Leicester hali si hali the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/11/epl-premier-league-round-up-manchester.html
0 Response to "EPL: Premier League round-up: Manchester City, Liverpool na Swansea zaishinda, Pardew njia panda na Leicester hali si hali"
Post a Comment