Title : EPL: Manchester United v Arsenal: Zlatan Ibrahimovic kuikosa Gunners, Alexis Sanchez arejea, Hector Bellerin nje
link : EPL: Manchester United v Arsenal: Zlatan Ibrahimovic kuikosa Gunners, Alexis Sanchez arejea, Hector Bellerin nje
EPL: Manchester United v Arsenal: Zlatan Ibrahimovic kuikosa Gunners, Alexis Sanchez arejea, Hector Bellerin nje
MSHAMBULIAJI wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic anatumikia adhabu ya kukosa mechi moja.
Wachezaji wanne wa United Luke Shaw, Marouane Fellaini, Antonio Valencia na Wayne Rooney ni majeruhi na huenda wakakosekana kwenye mchezo dhidi ya Arsenal.
Arsenal itamtumia Alexis Sanchez, ambaye alianza kikosi cha kwanza kwa Chile Jumanne iliyopita licha ya kusumbuliwa na matatizo ya afya mapema kwenye mapumziko ya kimataifa.
Mlinzi wa kulia Hector Bellerin ataukosa mchezo huo na atakuwa nje kwa wiki nne kwa sababu ya matatizo ya enka, wakati Santi Cazorla ataendelea kukosekana.
Manchester United v Arsenal
Uso-kwa-uso
- Arsenal haijashinda kwenye mechi tisa za mwisho za Premier League ilizotembelea Old Trafford, ikipoteza saba kati ya hizo.
- Hata hivyo, the Gunners ilishinda ugenini dhidi ya United kwenye FA Cup mwaka 2015.
Manchester United
- United inaweza kulinganisha ushindi wa tatu mfululizo kwenye ligi na nyumbani kwa mara ya kwanza tangu sawa na mbio hizo baina ya Februari na Aprili 1992.
- Kichapo kitawafanya wabaki kwenye pointi zao 18 na kuifikia rekodi yao mbaya kwa pointi chache baada ya 12 kwenye msimu wa Premier League, iliyoweka msimu wa 2004-05.
- Jose Mourinho hajawahi kupoteza mchezo wa Premier League dhidi ya Arsenal, akishinda mechi tano na sare sita katika mechi zake 11 zilizopita dhidi ya the Gunners.
- Wayne Rooney amefunga mabao 14 kwenye mashindano yote dhidi ya Arsenal wakati wa uchezaji wake. Ana rekodi nzuri dhidi ya Aston Villa, akiifunga mabao 15.
- Rooney alifunga bao lake la kwanza la Premier League dhidi ya Arsenal, wakati bao lake la kwanza la ligi akiwa na United na bao lake la 100 la Premier League pia lilikuwa dhidi ya the Gunners.
- Anahitaji mabao mawili kuifikia rekodi ya Bobby Charlton kuwa mfungaji wa muda wote wa Manchester United akiwa na mabao 249 kwenye mashindano yote.
Arsenal
- Ushindi pekee wa Arsene Wenger kwenye mechi 15 zilizopita akiwa meneja kwenye mashindano yote dhidi ya Jose Mourinho ulikuwa 2015 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii (D6, L8).
- Kichapo pekee cha Arsenal kwenye Premier League ugenini mwaka 2016 kilikuwa kutoka kwa Manchester United Februari.
- Imepoteza mechi moja pekee kati ya mechi 21 zilizopita.
- The Gunners ni moja kati ya timu mbili za Premier League ambayo haijawahi kuruhusu bao ndani ya dakika 15 za kwanza msimu huu, sanjari na West Brom.
Thus articles EPL: Manchester United v Arsenal: Zlatan Ibrahimovic kuikosa Gunners, Alexis Sanchez arejea, Hector Bellerin nje
that is all articles EPL: Manchester United v Arsenal: Zlatan Ibrahimovic kuikosa Gunners, Alexis Sanchez arejea, Hector Bellerin nje This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article EPL: Manchester United v Arsenal: Zlatan Ibrahimovic kuikosa Gunners, Alexis Sanchez arejea, Hector Bellerin nje the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/11/epl-manchester-united-v-arsenal-zlatan.html
0 Response to "EPL: Manchester United v Arsenal: Zlatan Ibrahimovic kuikosa Gunners, Alexis Sanchez arejea, Hector Bellerin nje"
Post a Comment