Title : Europa League: Manchester United 4-0 Feyenoord: United yanusa hatua ya 32
link : Europa League: Manchester United 4-0 Feyenoord: United yanusa hatua ya 32
Europa League: Manchester United 4-0 Feyenoord: United yanusa hatua ya 32
Wayne Rooney anakuwa mfungaji wa muda wote wa Manchester United kwenye mashindano ya Europe akiisaidia timu hiyo kuichapa Feyenoord mabao 4-0 na kuhuisha matumaini ya kutinga hatua ya mtoano wa Europa League wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Nahodha huyo wa Red Devils alifunga bao lake la 39 katika mashindano ya Ulaya alipoupiga mpira juu ya Brad Jones akiunganisha mpira uliorushwa na Zlatan Ibrahimovic - huku Feyenoord wakidai alikuwa ameotea.
Kisha Rooney akatengeneza bao la pili lililofungwa na Juan Mata.
Ushindi ulionekana njia ya United baada ya mlinda mlango wa zamani wa Liverpool Jones kubabatizwa na krosi ya Ibrahimovic na kujaa wavuni, na Jesse Lingard akafunga bao la nne dakika za lala salama na kumpa Jose Mourinho ushindi mkubwa akiwa kama meneja wa United.
Sare au ushindi dhidi ya Zorya Luhansk kwenye mchezo wa mwisho hatua ya makundi katika Kundi A Alhamisi, 8 Disemba utawapeleka United hatua ya 32.
Mkhitaryan ang'ara zaidi - dondoo
- Hiki kinakuwa kichapo kikubwa kwa Feyenoord kwenye Uefa Cup/Europa League. Mara ya mwisho kupigwa nyingi ilikuwa kichapo cha mabao 5-1 kutoka kwa Borussia Monchengladbach mwaka 1986.
- Henrik Mkhitaryan alikuwa na mashuti mengi - sita kwenye mchezo, mawili zaidi ya alivyopiga kwenye mchezo wa United kabla ya huu.
- Juan Mata amefunga katika mechi mfululizo kwa United kwa mara ya kwanza tangu Septemba 2015.
- United ilikuwa na mashuti 12 yaliyolenga lango dhidi ya Feyenoord, mengi zaidi kwenye mchezo mmoja katika mashindano yote msimu huu.
- Idadi hiyo ni kubwa kwa timu kwenye Europa League msimu huu.
- Feyenoord imeshinda mara moja katika mechi saba ilizotembelea England kwenye mashindano ya Ulaya (D2 L4).
- United haijafungwa kwenye mechi 14 za Ulaya ilizocheza Old Trafford (zikijumlishwa na mechi za kufuzu), ikishinda zote tatu za hatua ya makundi msimu huu.
Kifuatacho?
Manchester United itawaalika West Ham katika mechi zao mbili zijazo - kwenye Premier League Jumapili, na robo-fainali ya EFL Cup Jumatano.
Thus articles Europa League: Manchester United 4-0 Feyenoord: United yanusa hatua ya 32
that is all articles Europa League: Manchester United 4-0 Feyenoord: United yanusa hatua ya 32 This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article Europa League: Manchester United 4-0 Feyenoord: United yanusa hatua ya 32 the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/11/europa-league-manchester-united-4-0.html
0 Response to "Europa League: Manchester United 4-0 Feyenoord: United yanusa hatua ya 32"
Post a Comment