Title : League Cup: Manchester United v West Ham United: United kuwakosa Paul Pogba na Marouane Fellaini
link : League Cup: Manchester United v West Ham United: United kuwakosa Paul Pogba na Marouane Fellaini
League Cup: Manchester United v West Ham United: United kuwakosa Paul Pogba na Marouane Fellaini
VIUNGO Paul Pogba na Marouane Fellaini wataukosa mchezo wa robo-fainali ya EFL Cup kati ya Manchester United dhidi ya West Ham United katika dimba la Old Trafford kutokana na kutumikia adhabu.
Walioneshwa kadi ya tano ya manjano kila mmoja msimu huu kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye Premier League Jumapili.
Mshambuliaji wa West Ham Diafra Sakho, ambaye alifunga bao kwenye dimba a Old Trafford mwishoni mwa wiki, atakosekana kwa sababu ya majearaha.
Andy Carroll anakaribia kurejea kutoka kwenye majeraha ya goti wakati mlinzi Winston Reid atakuwepo baada ya adhabu.
Kiungo wa Manchester United Ander Herrera alisema timu yake inataka kulipa "kisasi" baada ya kushindwa kupata ushindi Jumapili.
"Ni ukweli kwamba tunacheza Jumatano, ambapo tutalipa kisasi," Mhispania huyo aliongeza. "Tunaweza kuigeuza bahati yetu kwenye mchezo ujao wa EFL Cup.
"Haijalishi mashindano, haijalishi mchezo, tunataka kushinda. Tunataka kupigania kila kitu na tunataka kuwafurahisha mashabiki wetu.
Boss wa West Ham Slaven Bilic alisema anaweza kufanya mabadiliko kadhaa kwenye kikosi chake lakini alikuwa na imani wachezaji watakaocheza wataisaidia Hammers kucheza nusu-fainali.
"Itatupa kujiamini zaidi kama tutashinda mchezo na tutafanya kila kitu kwa hilo," aliongeza Bilic.
"Kama tutabadili wachezaji wachache kama United watafanya, haitomaanisha tunakwenda kwa sababu ya kucheza mchezo.
"Ni robo-fainali na kutinga nusu-fainali ni kitu kikubwa na tuko nyuma kwa mechi mbili kutinga fainali."
Nusu-fainali nyingine kwa West Ham?
- West Ham inataka kutinga nusu-fainali ya League Cup kwa mara ya 10 katika historia yake, na ya kwanza tangu 2013/14.
- Manchester United na West Ham mara ya mwisho kukutana kwenye League Cup msimu wa 2010/11, ambapo Hammers ilishinda mabao 4-0 kwenye robo-fainali. Inabaki kuwa ushindi wao mkubwa zaidi dhidi ya timu ya Premier League katika mashindano.
- The Red Devils imepoteza mara moja pekee katika mara 24 ilizokuwa nyumbani kwenye League Cup dhidi ya timu-mwenza ya Premier League (W22 D1), ilichapwa 1-2 dhidi ya Chelsea Januari 2005.
- Jose Mourinho hajapoteza mchezo kwenye League Cup tangu Disemba 2013, akishinda minane na sare mbili tangu hapo.
- West Ham imeshinda mara mbili kati ya 11 iliyocheza ugenini dhidi ya mpinzani wa Premier League kwenye League Cup (L9), ikifungwa angalau bao moja kila mchezo.
- Ander Herrera na Marcus Rashford wanaungana kwa mabao mawili kwenye EFL Cup msimu huu; mengi zaidi ya wawili wengine kwenye mashindano hayo.
- Mark Noble ametoa assist mara mbili kwenye EFL Cup mwaka huu, wakati hakuna mchezaji yeyote kwenye robo-fainali aliyefanya hivyo.
Thus articles League Cup: Manchester United v West Ham United: United kuwakosa Paul Pogba na Marouane Fellaini
that is all articles League Cup: Manchester United v West Ham United: United kuwakosa Paul Pogba na Marouane Fellaini This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article League Cup: Manchester United v West Ham United: United kuwakosa Paul Pogba na Marouane Fellaini the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/11/league-cup-manchester-united-v-west-ham.html
0 Response to "League Cup: Manchester United v West Ham United: United kuwakosa Paul Pogba na Marouane Fellaini"
Post a Comment