Title : African Sports: Aubameyang, Mahrez na Mane wawania tuzo ya Caf
link : African Sports: Aubameyang, Mahrez na Mane wawania tuzo ya Caf
African Sports: Aubameyang, Mahrez na Mane wawania tuzo ya Caf
NYOTA wa Borussia Dortmund na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang angali katika mstari wa kutetea tuzo yake ya Mchezaji Bora wa mwaka wa Afrika baada ya kutajwa kuingia katika tatu bora ya tuzo hiyo inayotolewa na Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf).
PEA, 27, atapambana na winga wa Leicester City na Algeria Riyad Mahrez - mshindi wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika 2016 inayotolewa na Shirika la Utangazaji Uingereza, BBC - na winga wa Liverpool na Senegal Sadio Mane.
Kiungo wa Misri Mohamed Salah na nyota Islam Slimani wa Algeria wametolewa baada ya kutinga tano bora.
Caf ilithibitisha kwamba washindi watatangazwa kwenye sherehe zitakazofanyika Alhamisi, Januari 5 mjini Abuja, Nigeria.
Tuzo ya mwaka jana aliyoipata Aubameyang ilimaliza utawala wa kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure aliyeitwaa tuzo hiyo mara nne mfululizo.
Mahrez ana nafasi kubwa ya kuibuka kinara baada ya kuwa na mwaka mzuri wa 2016 ambao aliisaidia Leicester City kutwaa taji la Premier League na na kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka ya Wachezaji wa Uingereza.
Kiungo wa Zambia Rainford Kalaba, mshambuliaji wa Zimbabwe Khama Billiat na mlinda mlango wa Uganda Denis Onyango ni wachezaji watatu wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka kwa wachezaji wa ndani.
Orodha kamili ya wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa Afrika:
- Pierre-Emerick Aubameyang - Borussia Dortmund (Ujerumani) na Gabon
- Riyad Mahrez - Leicester City (England) na Algeria
- Sadio Mane - Liverpool (England) na Senegal
Orodha kamili ya wanaowania tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa Afrika (kwa wachezaji wa ndani):
- Denis Onyango - Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) na Uganda
- Khama Billiat - Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) na Zimbabwe
- Rainford Kalaba - TP Mazembe (DR Congo) na Zambia
Thus articles African Sports: Aubameyang, Mahrez na Mane wawania tuzo ya Caf
that is all articles African Sports: Aubameyang, Mahrez na Mane wawania tuzo ya Caf This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article African Sports: Aubameyang, Mahrez na Mane wawania tuzo ya Caf the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/african-sports-aubameyang-mahrez-na.html
0 Response to "African Sports: Aubameyang, Mahrez na Mane wawania tuzo ya Caf"
Post a Comment