Title : EPL: Bournemouth 4-3 Liverpool: The Cherries wamzima Klopp
link : EPL: Bournemouth 4-3 Liverpool: The Cherries wamzima Klopp
EPL: Bournemouth 4-3 Liverpool: The Cherries wamzima Klopp
Bournemouth ilitoka nyuma na kuichapa Liverpool mabao 4-3 kwenye Premier League.
The Cherries walipambana kutoka nyuma kwa mabao 2-0 kipindi cha kwanza na mabao 3-1 nyuma ndani ya dakika 15 kuelekea filimbi ya mwisho, huku bao la Nathan Ake dakika ya 93 likiihakikishia ushindi.
Sadio Mane aliifungia Reds bao la kuongoza alipomiliki mpira uliopigwa na Emre Can.
Wageni walionekana kumaliza mchezo baada ya Divock Origi kufunga bao la pili.
Bournemouth walimuingiza Ryan Fraser dakika ya 55 jambo lililosaidia sana Sekunde kadhaa baadaye James Milner alimuangusha kwenye box na Callum Wilson akafunga kwa mkwaju wa penalti.
Can akafanya matokeo kuwa mabao 3-1 kwa Reds lakini Fraser alifunga bao lake la kwanza la Premier League alipoungannisha krosi ya Wilson.
Mlinzi wa kati Steve Cook akaisawazishia Bournemouth alipounganisha krosi ya Fraser.
Ilionekana kama tamthiliya hadi dakika tatu za nyongeza ambapo Loris Karius kutema shuti la Cook na Ake akafunga.
Liverpool yadoda baada ya kuongoza kwa mabao mawili tena: dondoo za mechi
- The Cherries ilitoka nyuma kwa mabao mawili na kushinda mchezo wa Premier League kwa mara ya kwanza.
- Mechi mbili za kupoteza kwa timu iliyoongoza kwa mabao mawili mpaka mapumziko kwenye Premier League sasa inaihusisha na Liverpool ikipoteza kwa South Coast (pia mabao 2-3 v Southampton Machi 2016).
- Wachezaji wawili pekee wamefunga mabao zaidi kwenye mechi zao 13 za kwanza kwenye Premier League kwa Liverpool zaidi ya Mane (7) - Robbie Fowler (8) na Daniel Sturridge (10).
- The Reds imefunga mabao 19 kipindi cha kwanza kwenye Premier League msimu huu, matatu zaidi ya timu nyingine.
- Callum Wilson amefunga kwenye mechi tano kati ya tisa za Premier League alizoanza kwenye dimba la Vitality kwa Bournemouth (mabao matano).
- Hii ilikuwa mara ya nne chini ya Klopp kwamba Liverpool ilikuwa mbele kwa mabao mawili kwenye mchezo wa Premier League na kushindwa kuibuka washindi (2-2 v Sunderland, 2-3 v Southampton na 2-2 v Newcastle).
- Ryan Fraser ni mchezaji wa tatu wa Premier League msimu huu kufunga na kutoa assist kwenye mchezo akitokea kwenye benchi (Shaun Maloney na Robert Snodgrass kwa Hull ni wengine).
- Chini ya Klopp, Liverpool imeweka clean sheet nne kwenye mechi 23 za ugenini kwenye Premier League, ikifungwa mabao 38.
- Liverpool imepoteza mchezo wa Premier League kwa mabao 4-3 kwa mara ya kwanza tangu Novemba 2000 dhidi ya Leeds United.
Kifuatacho?
Bournemouth watakuwa njiani kuwafuata Burnley, ambao Howe alikuwa meneja baina ya vipindi viwili Cherries, Jumamosi kwenye Premier League. Liverpool itawaalika West Ham siku inayofuata.
Thus articles EPL: Bournemouth 4-3 Liverpool: The Cherries wamzima Klopp
that is all articles EPL: Bournemouth 4-3 Liverpool: The Cherries wamzima Klopp This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article EPL: Bournemouth 4-3 Liverpool: The Cherries wamzima Klopp the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/epl-bournemouth-4-3-liverpool-cherries.html
0 Response to "EPL: Bournemouth 4-3 Liverpool: The Cherries wamzima Klopp"
Post a Comment