Title : EPL: Premier League round-up: Chelsea yaongeza pengo, Liverpool yakamata nafasi ya pili na Manchester United yashinda usiku
link : EPL: Premier League round-up: Chelsea yaongeza pengo, Liverpool yakamata nafasi ya pili na Manchester United yashinda usiku
EPL: Premier League round-up: Chelsea yaongeza pengo, Liverpool yakamata nafasi ya pili na Manchester United yashinda usiku
Chelsea ilishinda mchezo wa 10 mfululizo kwenye Premier League na kuifanya iongoze msimamo kwa pointi sita.
Sunderland 0 - 1 Chelsea
Chelsea ilipata ushindi wa 10 mfululizo kwenye Premier League na kuongoza msimamo wa ligi hiyo kwa pointi sita zaidi.
Cesc Fabregas alifunga bao pekee kwa the Blues muda mfupi kabla ya mapumziko wakiendeleza kiwango chao kizuri chini ya boss Antonio Conte.
Kichapo kinaifanya Sunderland isalie mkiani kwa pointi nne kutoka eneo salama.
Middlesbrough 0 - 3 Liverpool
Liverpool ilipaa hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Premier League baada ya ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Middlesbrough kwenye mchezo uliopigwa Riverside Stadium.
Mabao mawili ya Adam Lallana na moja la Divock Origi yaliwahakikishia ushindi vijana wa Jurgen Klopp kurejea kwenye mstari na kuwapiku Arsenal kwa tofauti ya mabao.
Matokeo hayo yanaifanya Middlesbrough kukaa katika nafasi ya 17 na pointi tatu juu ya mstari wa hatari.
Manchester United imeanza kunusa top four baada ya ushindi wa dakika za lala salama katika mchezo uliopigwa Selhurst Park.
Paul Pogba aliipa Red Devils bao la kuongoza kabla ya James McArthur kuisawazishia Eagles. Lakini Zlatan Ibrahimovic aliihakikishia timu ya Jose Mourinho pointi tatu muhimu na kuwa nyuma ya top four kwa pointi sita nafasi ambayo inakaliwa na Manchester City kwa bao la dakika za lala salama.
Kufuatia kichapo, timu ya meneja Alan Pardew Palace inakaa pointi tatu juu ya timu tatu za mkiani.
Tottenham Hotspur 3 - 0 Hull City
Tottenham ilihuisha matumaini yao ya kuingia tena top four baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Hull City katika mchezo uliopigwa White Hart Lane.
Christian Eriksen alifunga mara mbili kabla ya Victor Wanyama kufunga bao la tatu katika mchezo ambao vijana wa Mauricio Pochettino walikuwa na kiwango kizuri.
Matokeo hayo yanawaacha the Tigers katika nafasi ya 19 na pointi tatu kutoka sehemu salama.
Manchester City 2 - 0 Watford
Manchester City ilifunga zaidi mkanda katika nafasi ya nne baada ya kuichapa Watford katika mchezo uliopigwa Etihad Stadium.
Pablo Zabaleta na David Silva waliifungia City kuisaidia timu ya Pep Guardiola kusahau wikiendi mbaya ambayo walidhalilishwa na Leicester.
The Hornets wanakaa katika nafasi ya 11 na pointi tisa kutoka ukanda mbaya.
West Ham United 1 - 0 Burnley
West Ham ilipata ushindi wao wa kwanza kwenye mechi saba wakiichapa Burnley katika mchezo uliopigwa London Stadium.
Mark Noble alifunga bao pekee kwa the Hammers baada ya kuunganisha mpira wa penalti aliyopiga mwenyewe. Vijana wa Sean Dyche walijaribu kuwa wasumbufu, lakini vijana wa Slaven Bilic waligangamala wakihitaji ushindi.
Kwa matokeo hayo Burnley wanakaa katika nafasi ya 13 pointi tano kutoka ukanda wa kushuka daraja.
West Bromwich Albion 3 - 1 Swansea City
West Brom iliendeleza kiwango chao kizuri wakiibuka na ushindi dhidi ya Swansea katika dimba la Hawthorns.
Salomon Rondon alifunga hat-trick kwa the Baggies kabla ya Wayne Routledge kuifungia timu ya Bob Bradley bao la kufutia machozi.
Vijana wa Tony Pulis wanapaa hadi nafasi ya saba wakati Swansea wakisalia katika eneo la kushuka daraja na pointi tatu chini ya mstari.
Stoke City 0 - 0 Southampton
Stoke na Southampton zilimaliza dakika 90 kwa sare katika mchezo uliopigwa Bet365 Stadium.
Timu mbili hizo za katikati ya msimamo zilishindwa kutambiana na kuzifanya zikiwa pointi 10 katika eneo la nafasi za soka la Europe.
Thus articles EPL: Premier League round-up: Chelsea yaongeza pengo, Liverpool yakamata nafasi ya pili na Manchester United yashinda usiku
that is all articles EPL: Premier League round-up: Chelsea yaongeza pengo, Liverpool yakamata nafasi ya pili na Manchester United yashinda usiku This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article EPL: Premier League round-up: Chelsea yaongeza pengo, Liverpool yakamata nafasi ya pili na Manchester United yashinda usiku the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/epl-premier-league-round-up-chelsea.html
0 Response to "EPL: Premier League round-up: Chelsea yaongeza pengo, Liverpool yakamata nafasi ya pili na Manchester United yashinda usiku"
Post a Comment