Title : EPL: West Bromwich Albion v Manchester United: United kumkosa 'fundi' Henrik Mkhitaryan
link : EPL: West Bromwich Albion v Manchester United: United kumkosa 'fundi' Henrik Mkhitaryan
EPL: West Bromwich Albion v Manchester United: United kumkosa 'fundi' Henrik Mkhitaryan
MLINZI wa West Brom ambaye zamani alikuwa anakipiga Manchester United Jonny Evans anakumbana na kukosa uimara wa mchezo baada ya kuukosa mchezo wa katikati ya wiki ambapo walishinda dhidi ya Swansea kwa sababu ya majeraha ya kifundo cha mguu.
Craig Dawson atakuwepo baada ya kutumikia adhabu ya kukosa mechi moja kutokana na kadi tano za manjano.
Henrik Mkhitaryan atakosekana kwa upande wa Manchester United baada ya kuondolewa na machela kutokana kuumia enka kwenye mchezo dhidi ya Spurs ambapo United walishinda kwa bao 1-0.
Antonio Valencia amerejea baada ya kutumikia adhabu lakini Eric Bailly yupo shakani kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya goti.
West Bromwich Albion v Manchester United
Uso-kwa-uso
- West Brom imeshinda mara tatu kati ya mechi sita za mwisho ilizokutana na Manchester United baada ya kucheza mara 18 bila ushindi.
- Hata hivyo, Manchester United imeshinda mara tisa kati ya mara 12 za ligi ilizotembelea The Hawthorns, huku kichapo cha mwisho wakikipata msimu uliopita.
- Albion wanaweza kuvuna ushindi mfululizo dhidi ya Manchester United kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1980.
West Bromwich Albion
- The Baggies wanataka kuifikia rekodi yao ya kushinda mechi nne mfululizo za Premier League katika uwanja wao wa nyumbani.
- Wamepoteza mara moja kati ya mechi sita za ligi.
- West Brom imefunga mabao tisa ya vichwa kwenye Premier League msimu huu, mengi zaidi sanjari na Crystal Palace.
- Tony Pulis anaweza kuwa meneja wanne, baada ya Alan Pardew, Mark Hughes na Pep Guardiola, kushinda zaidi ya mechi mbili za ligi dhidi ya Jose Mourinho.
- Salomon Rondon amefunga mabao 16 ya Premier League tangu kuanza kwa msimu uliopita - mabao 11 zaidi ya mchezaji yeyote wa West Brom.
Manchester United
- Manchester United imepoteza mchezo mmoja katika mechi 11 za ligi (W4, D6).
- United inaingia uwanjani ikipata ushindi mfululizo kwenye ligi - kiwango chao kizuri tangu iliposhinda mechi tatu za mwanzo wa msimu.
- Kama Manchester United watapoteza, wataifikia rekodi yao ya pointi chache zaidi baada ya mechi 17 za msimu wa Premier League: 27 msimu wa 1992-93 na 2001-02.
- Wayne Rooney amefunga mabao saba na kutengeneza manne katika mechi tisa za ligi dhidi ya West Brom. Pungufu ya bao moja kuifikia rekodi ya klabu iliyowekwa na Sir Bobby Charlton ya mabao 249 kwenye mashindano yote.
Thus articles EPL: West Bromwich Albion v Manchester United: United kumkosa 'fundi' Henrik Mkhitaryan
that is all articles EPL: West Bromwich Albion v Manchester United: United kumkosa 'fundi' Henrik Mkhitaryan This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article EPL: West Bromwich Albion v Manchester United: United kumkosa 'fundi' Henrik Mkhitaryan the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/epl-west-bromwich-albion-v-manchester.html
0 Response to "EPL: West Bromwich Albion v Manchester United: United kumkosa 'fundi' Henrik Mkhitaryan"
Post a Comment