Title : Fifa News: Shirikisho la vilabu Ulaya laigomea Fifa kuongeza timu Kombe la Dunia
link : Fifa News: Shirikisho la vilabu Ulaya laigomea Fifa kuongeza timu Kombe la Dunia
Fifa News: Shirikisho la vilabu Ulaya laigomea Fifa kuongeza timu Kombe la Dunia
CHAMA kinachowakilisha klabu zinazoongoza barani Europe kimakataa upanuzi wa fainali za Kombe la Dunia.
Mapema mwezi huu, rais wa Fifa Gianni Infantino alipendekeza kuongeza timu kwenye fainali za Kombe la Dunia hadi kufikia 48 ambazo zingalicheza katika makundi 16 yenye nchi tatu kila moja.
Shirikisho la Klabu barani Ulaya (ECA) linasema idadi ya michezo inayocheza kwa mwaka tayari "imevuka levo isiyokubalika".
"Tunaiomba Fifa kutoongeza idadi ya washiriki wa Kombe la Dunia," alisema mwenyekiti wa ECA Karl-Heinz Rummenigge.
Halmashauri ya Fifa italijadili pendekezo la Infantino katika mkutano utakaofanyika 9 Januari lakini rais huyo mwenye umri wa miaka 46 alifanya upanuzi wa baadhi ya maeneo katika ilani yake kwa sababu anataka kuruhusu nchi nyingi zaidi kupata nafasi ya kushindana kwenye mashindano hayo makubwa.
Mara ya mwisho kuongeza idadi ya timu zinazoshiriki Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 1998 wakati ambapo mashindano hayo yalishuhudia timu 32 badala ya 24 lakini mabadiliko yoyote katika muundo wa sasa huenda ukaanza kutekelezwa katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2026.
Rummenigge aliongeza: "Tunatakiwa kuelekeza nguvu zaidi katika michezo tena. Siasa na biashara zisiwe kipaumbele kwenye soka."
ECA inawakilisha zaidi ya klabu 200, zikiwamo Real Madrid, Barcelona, Juventus, Bayern Munich, Manchester United na Chelsea.
Thus articles Fifa News: Shirikisho la vilabu Ulaya laigomea Fifa kuongeza timu Kombe la Dunia
that is all articles Fifa News: Shirikisho la vilabu Ulaya laigomea Fifa kuongeza timu Kombe la Dunia This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article Fifa News: Shirikisho la vilabu Ulaya laigomea Fifa kuongeza timu Kombe la Dunia the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/fifa-news-shirikisho-la-vilabu-ulaya.html
0 Response to "Fifa News: Shirikisho la vilabu Ulaya laigomea Fifa kuongeza timu Kombe la Dunia"
Post a Comment