Title : La Liga: Barcelona v Real Madrid: Ukizubaa umelizwa
link : La Liga: Barcelona v Real Madrid: Ukizubaa umelizwa
La Liga: Barcelona v Real Madrid: Ukizubaa umelizwa
MIAMBA miwili ya soka Duniani, Barcelona na Real Madrid, zitakutana. Mechi, ambayo hujulikana kama El Clasico, itapigwa kwenye dimba la Camp Nou Jumamosi ikiwa Barcelona ni mwenyeji wakiwaalika mahasimu wao Real Madrid.
Mashabiki wa soka duniani wanasubiri kwa hamu mchezo unaotajwa kuwa bora na mkali katika sayari hii, Barcelona vs. Real Madrid. Mchezo huo pia utawahusishwa wachezaji wakubwa wawili duniani Messi na Ronaldo ambao watakutana uso-kwa-uso.
El Clasico ya Jumamosi itakuwa muhimu kwa timu zote kuelekea mawindo ya ubingwa msimu huu. Ushindi ni muhimu kwa Barcelona kama wana matumaini ya kushinda La Liga msimu huu. Wako nyuma kwa pointi sita dhidi ya mahasimu wao Real Madrid, baada ya mechi 13, na kichapo Jumamosi kitakuwa ni pigo kubwa katika harakati zao za kutetea taji la La Liga. Real Madrid wanafurahia mbio zao za ushindi wakiwa bado hawajapoteza mchezo hata mmoja msimu huu. The Whites wana rekodi nzuri ya kutofungwa kwenye mechi zao 31, na watakuwa na lengo la kulinda rekodi hiyo kwa kuwachapa mahasmu wao kwenye ardhi yao.
Ushindi kwa Real utawaweka juu ya Barcelona kwa pointi tisa zaidi, na kuwafanya kuukaribia ubingwa wa Uhispania kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitano.
Timu mwenyeji, Barcelona, itaingia uwanjani baada ya sare mbili mfululizo kwenye La Liga, wakati wapinzani wao, Real Madrid, wameshinda mechi nne mfululizo.
Mara ya mwisho timu hizi kukutana Camp Nou, Madrid iliichabanga Barca mabao 2-1, shukrani kwa bao la ushindi kutoka kwa Cristiano Ronaldo dakika za lala salama.
Taarifa za timu: Barcelona
Baada ya kuwapumzisha wachezaji wake muhimu kwenye mchezo wa Copa Del Rey dhidi ya Hercules, Luis Enrique anatarajia kukijaza kikosi chake dhidi ya Los Blancos. Habari njema kwa Barcelona ni kwamba hakuna majeruhi wapya baada ya mchezo wa Hercules ambayo yanaweza kukiathiri kikosi.
Lionel Messi, Luis Suarez, na Neymar Jr watakuwa mstari wa mbele kuongoza mashambulizi kama kawaida yao.
Kwenye mchezo dhidi ya Real Sociedad uliopigwa Anoeta, ilikuwa ni siku mbaya kwa muungano unaojulikana kama MSN.
Kurejea kwa Messi, Neymar, na Suarez kutatoa shida sana kwa safu ya ulinzi wa Real Madrid. Hivyo, Zinedine Zidane ana kazi ngumu kuzuia mashambulizi kutoka kwa muungano huo.
Katika upande mwingine, walinzi wa kati Gerard Pique na Javier Mascherano watakuwa katika ubora wao kuzuia mawimgi ya mashambulizi ya mafowadi wa Real Madrid, yakiongozwa na Cristiano. Pia kurejea kwa kiungo mpishi Andres Iniesta baada ya kukosekana kwa miezi miwili kutaongeza hamasa kwa Catalans. Barcelona imekuwa na wakati mgumu siku za hivi karibuni hasa kutokana na kumkosa mshindi huyo wa Kombe la Dunia. Hivyo, kujumuishwa kwake kwenye timu kutaifanya Barca kutawala kwenye kiungo.
Jambo baya linaloikumba Barcelona msimu huu ni kiwango kibovu cha Sergio Busquets. Kuwepo kwa Iniesta sanjari naye kunaweza kuwa na jambo muhimu.
Kikosi cha Barcelona kinachotabiriwa dhidi ya Real Madrid (4-3-3)
ter Stegen – Roberto, Pique, Mascherano, Alba – Rakitic, Busquets, Iniesta – Messi, Suarez, Neymar
Taarifa za timu: Real Madrid
Real Madrid haijawa na bahati msimu huu linapokuja suala la majeraha kwa wachezaji wake muhimu.
Nyota wa Wales Gareth Bale anasumbuliwa na enka ambayo itamuweka nje ya uwanja angalau kwa miezi mitatu. Kiungo Toni Kroos pia ataukosa mchezo dhidi ya Barcelona kutokana na majeraha aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Leganes.
Usajili mpya Alvaro Morata, ambaye ni mmoja wa wachezaji bora kwenye kikosi cha Los Blancos, pia atakosekana kutokana na majeraha aliyoyapata wakati wa mapumziko ya kimataifa.
Hata hivyo, habari njema kwa Zinedine Zidane ni kwamba kiungo 'mkata umeme' Casemiro amerejea kwenye timu baada ya wiki kadhaa za kuuguza majeraha. Anatarajia kuwa muhimu zaidi katika eneo la kiungo wa Real Madrid kuharibu mipango ya Barca.
Kwenye Clasico iliyopita, Casemiro aliweza kumdhibiti Messi. Hivyo, kuwepo kwake kwenye mchezo huu kutaisaidia sana Real.
Katika wiki za karibuni, mashabiki wa Real Madrid wamekuwa na furaha baada ya kurejea kwa kiwango cha kiongozi wao, Ronaldo. Nahodha huyo wa Ureno amezifumania nyavu katika mechi za hivi karibuni, na dhidi ya Barca, anatarajia kuing'arisha Real.
Wote - Messi na Ronaldo wametajwa kuwania Ballon d’Or, na kiwango kizuri kwenye mchezo huu kitasiadia bila shaka kujiweka kazirbu zaidi na tuzo hiyo.
Kikosi cha Real Madrid kinachotabiriwa dhidi ya Barcelona (4-3-3)
Navas – Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo – Modric, Kovacic, Casemiro – Isco, Ronaldo, Benzema
Navas – Carvajal, Pepe, Ramos, Marcelo – Modric, Kovacic, Casemiro – Isco, Ronaldo, Benzema
Lionel Messi v Cristiano Ronaldo: Uso-kwa-uso
Messi v Real Madrid
- Messi ni mfungaji kinara kwenye historia ya El Clasico, akifunga mabao 21.
- Messi ametoa assist 13 katika mechi 32 alizocheza dhidi ya Real Madrid.
- Ameshinda mechi 15 za El Clasico. (47%)
- Messi amefunga 57% ya mabao yake katika dimba la Bernabeu.
- Leo hajafunga katika mechi tano za mwisho za Clasico.
Ronaldo v Barcelona
- Kama Messi, Ronaldo amefunga mabao mengi zaidi ugenini – 10 kati ya mabao 16 ya Clasico amefunga katika dimba la Camp Nou.
- Ni Alfredo Di Stefano (18) amefunga mabao mengi zaidi dhidi ya Barcelona kwa Real Madrid zaidi ya Cristiano.
- Ronaldo ana rekodi mbaya ya ushindi dhidi ya Barca akishinda mara saba katika mechi 25. (28%)
- Nyota huyo wa Ureno ana assist moja pekee kwenye mechi 25 za Clasico, 12 pungufu ya hasimu wake Messi.
Dondoo za Ronaldo v Messi zimetolewa na Goal.
Angalia vita ya Messi v Ronaldo
Barcelona v Real Madrid: Uso-kwa-uso
Jumla ya mechi: 231
Barcelona imeshinda: 90
Real Madrid imeshinda: 93
Sare: 48
Barcelona v Real Madrid: TV na Channel zitakazoonesha
Marekani, mchezo utaoneshwa kupitia beIN SPORTS en Espanyol, fuboTV, beIN SPORTS CONNECT U.S.A., na beIN SPORTS USA. Lakini Uingereza, mchezo hautooneshwa moja kwa moja kutokana na muda wa mechi. Kwa sehemu nyingine, bofya kiunganishi hiki kujua zaidi.
Dondoo muhimu
- Real Madrid haijafungwa katika mechi 31 zilizopita kwenye mashindano yote.
- Real Madrid imeshinda mchezo El Clasico wa hivi karibuni, waliichapa Barca mabao 2-1.
- Barcelona haijafungwa kwenye mechi 29 kati ya 32 za La Liga ilizocheza nyumbani.
- Fowadi wa Barca Messi hajafunga bao kwenye El Clasico tangu 2014.
Thus articles La Liga: Barcelona v Real Madrid: Ukizubaa umelizwa
that is all articles La Liga: Barcelona v Real Madrid: Ukizubaa umelizwa This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article La Liga: Barcelona v Real Madrid: Ukizubaa umelizwa the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/la-liga-barcelona-v-real-madrid.html
0 Response to "La Liga: Barcelona v Real Madrid: Ukizubaa umelizwa"
Post a Comment