Title : La Liga News: Lionel Messi na Luis Suarez kwenye mazungumzo ya mkataba mpya na Barca
link : La Liga News: Lionel Messi na Luis Suarez kwenye mazungumzo ya mkataba mpya na Barca
La Liga News: Lionel Messi na Luis Suarez kwenye mazungumzo ya mkataba mpya na Barca
FOWADI wa Barcelona Lionel Messi ameanza mazungumzo na mabingwa watetezi wa La Liga kuhusu mkataba mpya, wakati mshambuliaji Luis Suarez anatarajia kusaini mkataba mpya hadi 2022.
Nahodha wa Argentina Messi, 29, tayari ana mkataba na klabu hiyo hadi June 2018, ma boss wa Barca Luis Enrique alisema "anafurahia" namna mazungumzo yanvyokwenda.
"Iinanifanya nitulie zaidi," aliongeza.
Mshambuliaji wa Uruguay Suarez, 29, anakaribia kuongeza muda wake wa kuishi Nou Camp.
Mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool ameshinda mataji mawili ya La Liga na Champions League mara moja tangu alipotua Barcelona July 2014 kwa ada ya paundi 75m.
"Imekamilika, ni maelezo machache tu yanahitaji kuwekwa sawa na tutatangaza katika ama siku au wiki chache zijazo," alisema rais wa Barca Josep Maria Bartomeu.
"Tunataka Luis Suarez abaki klabuni kwa miaka mingi zaidi. Kwetu, ni muhimu sana."
Suarez alishinda Golden Shoe Ulaya msimu uliopita - ambayo hutolewa kwa mfungaji bora wa Europe katika soka la ndani - baada ya kufunga mabao 40 ya ligi.
Yeye, Messi - mfungaji kinara wa muda wote wa Barca, na Neymar walifunga jumla ya mabao 131 kwenye mashindano yote ambapo walishinda La Liga na Copa del Rey.
Bartomeu, akizungumza na kituo cha radio Cadena Celeste ya Uruguay, aliongeza: "Itakuwa ni zawadi kubwa ya Christmas, siyo kwa Luis ambaye tayari ameshajua kuwa ataendelea hapa, bali kwa mashabiki wa soka.
"Anaunda utatu tuliokuwa nao, ambao unasaidia timu nzima."
Thus articles La Liga News: Lionel Messi na Luis Suarez kwenye mazungumzo ya mkataba mpya na Barca
that is all articles La Liga News: Lionel Messi na Luis Suarez kwenye mazungumzo ya mkataba mpya na Barca This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article La Liga News: Lionel Messi na Luis Suarez kwenye mazungumzo ya mkataba mpya na Barca the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/la-liga-news-lionel-messi-na-luis.html
0 Response to "La Liga News: Lionel Messi na Luis Suarez kwenye mazungumzo ya mkataba mpya na Barca"
Post a Comment