Title : Tetesi za usajili: Paris St-Germain kutoa ofa ya paundi 50m kwa Dele Alli, Depay, Young kuondoka United, Tevez kwenda Uchina, Aubameyang na Madrid mambo yameiva
link : Tetesi za usajili: Paris St-Germain kutoa ofa ya paundi 50m kwa Dele Alli, Depay, Young kuondoka United, Tevez kwenda Uchina, Aubameyang na Madrid mambo yameiva
Tetesi za usajili: Paris St-Germain kutoa ofa ya paundi 50m kwa Dele Alli, Depay, Young kuondoka United, Tevez kwenda Uchina, Aubameyang na Madrid mambo yameiva
MABINGWA wa Ufaransa Paris St-Germain inataka kutoa ofa ya paundi 50m kuinasa saini ya kiungo wa Tottenham na England Dele Alli, 20. (Daily Mirror)
Everton inataka kujaribu kumsajili winga wa Leicester City Demarai Gray, 20, Januari baada ya kumpoteza Yannick Bolasie aliyepata majeraha, ambayo yatamuweka nje kwa mwaka mzima. (Daily Mirror)
Everton pia inavutiwa na fowadi wa Manchester United Memphis Depay, 22, na mshambuliaji wa Napoli Manolo Gabbiadini, 25, ambaye huenda akawagharimu paundi 18m. (Sun)
Watford, West Brom, Swansea na Everton zinamuwinda winga wa Manchester United Ashley Young, 31. (Manchester Evening News)
Real Madrid na Bayern Munich zinapambana kuiwania saini ya mshambuliaji wa AIK Alexander Isak, 17, ambaye anawindwa pia na Chelsea, Manchester City na West Ham. (Marca)
Mshambuliaji wa Boca Juniors Carlos Tevez, 32, huenda akakubali ofa ya paundi 33m kutoka timu ya Gus Poyet Shanghai Shenhua, lakini pia anaweza kustaafu. (Goal.com)
Valencia inaweza kujaribu kumsajili fowadi wa Italia Simone Zaza, 25, anayecheza kwa mkopo katika klabu ya West Ham akitokea Juventus, Januari. (Superdeporte, via ESPN)
Borussia Dortmund imekubaliana na Real Madrid kuwa itawaarifu wahispania hao kabla ya kumuuza mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang, 27, kiungo Julian Weigl, 21, au Ousmane Dembele, 19. (Marca)
Arsenal, Manchester United, Manchester City, Tottenham na West Ham zinapigania saini ya mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe, 17. (HITC)
Mlinzi wa Chelsea Branislav Ivanovic, 32, hatoondoka klabuni hapo Januari, licha ya kuwindwa na mabingwa Italia Juventus. (Bleacher Report)
Manchester City imeduwazwa na mlinzi wake Eliaquim Mangala, 25, kurejea tena sokoni huku klabu inayoichezea kwa mkopo Valencia ikikataa kumnunua moja kwa moja kwa paundi 15m. (Sun)
Mshambuliaji wa Leicester City Leonardo Ulloa, 30, ambaye anawindwa na Sunderland, anajiandaa kuondoka klabuni hapo kwenda Uchina. (Sunderland Echo)
Chelsea inakumbana na ushindani kutoka kwa Tottenham na Juventus kumuwania kiungo wa Atalanta Franck Kessie, 19. (Gianluca Di Marzio, via Daily Star)
Thus articles Tetesi za usajili: Paris St-Germain kutoa ofa ya paundi 50m kwa Dele Alli, Depay, Young kuondoka United, Tevez kwenda Uchina, Aubameyang na Madrid mambo yameiva
that is all articles Tetesi za usajili: Paris St-Germain kutoa ofa ya paundi 50m kwa Dele Alli, Depay, Young kuondoka United, Tevez kwenda Uchina, Aubameyang na Madrid mambo yameiva This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article Tetesi za usajili: Paris St-Germain kutoa ofa ya paundi 50m kwa Dele Alli, Depay, Young kuondoka United, Tevez kwenda Uchina, Aubameyang na Madrid mambo yameiva the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/tetesi-za-usajili-paris-st-germain.html
0 Response to "Tetesi za usajili: Paris St-Germain kutoa ofa ya paundi 50m kwa Dele Alli, Depay, Young kuondoka United, Tevez kwenda Uchina, Aubameyang na Madrid mambo yameiva"
Post a Comment