Title : UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: Real Madrid v Borussia Dortmund: Ni kama fainali - Zidane
link : UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: Real Madrid v Borussia Dortmund: Ni kama fainali - Zidane
UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: Real Madrid v Borussia Dortmund: Ni kama fainali - Zidane
MCHEZO wa Real Madrid kwenye Champions League Kundi F dhidi ya Borussia Dortmund Jumatano ni "kama fainali", anasema meneja Zinedine Zidane.
Timu zote zinapambana kuwania uongozi wa kundi hilo ingawa tayari zimeshafuzu hatua ya mtoano.
Hata hivyo, Dortmund inaongoza msimamo na ina pointi mbili juu ya Real, ambayo italazimika kushinda ili kumaliza kileleni.
"Hatutokuwa lele mama. Tunacheza ili tushinde," alisema Zidane.
"Tunacheza fainali, mchezo ambao utaamua nani ataongoza kundi na tuko nyumbani hivyo ni wazi tunataka kucheza vizuri zaidi."
Fowadi wa Wales Gareth Bale ni mchezaji pekee wa Real kuukosa mchezo huo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 atakosekana kwa miezi minne baada ya kufanyiwa upasuaji wa enka 29 Novemba.
Kiungo wa Real Toni Kroos amerejea baada ya kuumia mguu wakati fowadi Alvaro Morata amepona pia majeraha yaliyokuwa yanamsumbua.
Mechi nyingine kwenye Champions League ni; CSKA Moscow itakuwa ugenini Wimbley kuwafuata Tottenham huku FC Porto wakiwa wenyeji wa Leicester City wakati Sevilla itasafiri nchini Ufaransa kukabiliana na Lyon na Bayer Leverkusen wakiwakaribisha Monaco.
Legia Warsaw watakuwa wenyeji wa Sporting Lisbon wakalti Club Brugge wakiwakaribisha FC Copenhagen na Dinamo Zagreb wakiwa wageni wa Juventus.
Champions League - nani atafuzu? |
---|
Kundi A: PSG na Arsenal, Europa League (EL) - Ludogorets |
Kundi B: Benfica na Napoli, EL - Besiktas |
Kundi C: Barcelona na Manchester City, EL - Borussia Monchengladbach |
Kundi D: Atletico Madrid na Bayern Munich, EL - FC Rostov |
Kundi E: Monaco na Bayer Leverkusen |
Kundi F: Borussia Dortmund na Real Madrid |
Kundi G: Leicester na moja kati ya FC Porto au FC Copenhagen |
Kundi H: Juventus na moja kati ya Sevilla au Lyon |
Thus articles UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: Real Madrid v Borussia Dortmund: Ni kama fainali - Zidane
that is all articles UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: Real Madrid v Borussia Dortmund: Ni kama fainali - Zidane This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: Real Madrid v Borussia Dortmund: Ni kama fainali - Zidane the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/uefa-8-viwanjani-leo-uefa-match-preview_6.html
0 Response to "UEFA: 8 viwanjani leo UEFA: Match Preview: Real Madrid v Borussia Dortmund: Ni kama fainali - Zidane"
Post a Comment