VPL: Yanga SC v African Lyon: Yanga kuiengua Simba kileleni?

VPL: Yanga SC v African Lyon: Yanga kuiengua Simba kileleni? - Hallo friend ALL NEW, In the article you read this time with the title VPL: Yanga SC v African Lyon: Yanga kuiengua Simba kileleni?, we have prepared well for this article you read and download the information therein. hopefully fill posts Article Culinary, Article Culture, Article Economy, Article Politics, Article Sports, Article The latest, Article Updated, we write can understand. Well, happy reading.

Title : VPL: Yanga SC v African Lyon: Yanga kuiengua Simba kileleni?
link : VPL: Yanga SC v African Lyon: Yanga kuiengua Simba kileleni?

Read also


VPL: Yanga SC v African Lyon: Yanga kuiengua Simba kileleni?

TIMU ya Yanga leo itakuwa na kibarua kigumu cha kuusaka uongozi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itakapoivaa African Lyon kwenye mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Yanga itaingia kwenye mchezo huo, ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya JKT Ruvu Jumamosi iliyopita na kufanikiwa kukaa kileleni kwa muda kabla ya kutolewa na Simba Jumapili.
Mabingwa watetezi na wa kihistoria katika soka la Tanzania, watapambana na Lyon, wakiwa katika nafasi ya pili ikijikusanyia pointi 36, baada ya mechi 16 wakati Lyon wakiwa nafasi ya 11 na pointi zao 14 walizozipata baada ya mechi 16.
Katika mchezo wa awali Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, hivyo ni wazi Lyon hawatokubali kupoteza pointi zote sita kwa Yanga msimu huu.
Lyon pamoja na kuwa moja ya timu zilizofanya vibaya kwenye mzunguko wa kwanza, lakini imejiwekea rekodi ya pekee, baada ya kuwa timu ya kwanza kuwafunga vinara Simba lakini ndiyo timu ambayo imeweza kuilazimisha sare timu tajiri ya Azam katika michezo yote miwili licha ya timu hiyo kujaa nyota wa kigeni kutoka mataifa ya Ghana na Cameroon.
Kikosi cha Yanga kitaingia kwenye mchezo wa leo huku kikitoka kwenye mgomo wa wachezaji waliokuwa hawajalipwa mishahara yao mwezi Novemba na kusababisha kushindwa kufanya mazoezi kwa siku mbili.
Tayari uongozi umeshamaliza tatizo hilo na timu ilirejea mazoezini kabla ya mchezo huo na lengo la kocha Lwandamina ni kuhakikisha wanashinda mchezo huo ili kuwapa presha Simba wanaoongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi mbili.
Katika mchezo wa leo, kocha Lwandamina anatarajia kumuanzisha kiungo mpya aliyemsajili kwenye dirisha dogo Justine Zullu maarufu kama ‘Mkata Umeme’ ambaye aliukosa mchezo wa kwanza baada ya kutokuwa na kibali cha kufanyia kazi.
Kikosi cha Lwandamina hakitarajiwi kuwa na mabadiliko makubwa na kile kilichoanza mechi iliyopita dhidi ya JKT Ruvu, na ataendelea kumtumia nahodha wake Haruna Niyonzima kama mchezesha timu ili kupata mabao.
Simon Msuva ambaye alifunga mabao mawiili kwenye mchezo uliopita anatarajiwa kuanza kikosi cha kwanza sambamba na Donald Ngoma na Hamis Tambwe ambao mchezo uiopita walitoka kapa licha ya kupata nafasi nyingi za kufunga.
Kocha huyo ataendelea kuutumika mfumo wake wa 4-3-3, ambao umekuwa ukimpa mafanikio tangu akiwa anaifundisha Zesco United ya Zambia na kuifikisha hatua ya nusu-fainali ya Klabu Bingwa Afrika.
Nao African Lyon pamoja na kuwasumbua Azam katika mchezo uliopita na kulazimishwa sare ya bila kufungana lakini hawapewi nafasi kubwa ya kuwasumbua Yanga ambao wanaonekana kuwa na mifumo mingi ya kiuchezaji ambayo imekuwa ikiwasaidia kupata matokeo.
Tegemeo kubwa la Lyon ni mlinda mlango kutoka Cameroon, ambaye alionesha kiwango cha juu dhidi ya Azam ambao walikuwa wakiwatumia nyota sita wapya waliowasajili kwenye dirisha dogo.


Thus articles VPL: Yanga SC v African Lyon: Yanga kuiengua Simba kileleni?

that is all articles VPL: Yanga SC v African Lyon: Yanga kuiengua Simba kileleni? This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.

You are now reading the article VPL: Yanga SC v African Lyon: Yanga kuiengua Simba kileleni? the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/vpl-yanga-sc-v-african-lyon-yanga.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "VPL: Yanga SC v African Lyon: Yanga kuiengua Simba kileleni?"

Post a Comment