Title : Copa del Rey: Athletic Bilbao 2-1 Barcelona: Barca yachapwa na wachezaji tisa
link : Copa del Rey: Athletic Bilbao 2-1 Barcelona: Barca yachapwa na wachezaji tisa
Copa del Rey: Athletic Bilbao 2-1 Barcelona: Barca yachapwa na wachezaji tisa
Athletic Bilbao ilipata ushindi katika mchezo wa kwanza wa Copa del Rey dhidi ya Barcelona kwa mabao 2-1 hatua ya 16 licha ya kumaliza mchezo wakiwa tisa uwanjani.
Mabao mawili ndani ya dakika tatu kipindi cha wanza yaliyofungwa na Aritz Aduriz na Inaki Williams yaliwaweka mbele wenyeji dhidi ya mabingwa wa 2016.
Lionel Messi akaifungia Barca kwa mpira wa free-kick baada ya mapumziko.
Messi pia akagonga mwamba dakika za lala salama baada ya Raul Garcia na Ander Iturraspe kuoneshwa kadi nyekundu.
"Tulipambana mwanzoni," alisema meneja wa Barca Luis Enrique.
"Kipindi cha pili tulielekeza nguvu katika kile tulichotakiwa kufanya, mchezo wetu, na nadhani tulifanya vya kutosha."
Mafowadi Messi, Luis Suarez na Neymar walianza kikosi cha kwanza licha ya kurejea kwenye mazoezi Jumatatu kufuatia mapumziko.
Hii ni mara ya sita Barca na Athletic kukutana katika mashindano haya katika misimu tisa, zikiwemo fainali tatu.
Hakuna timu zaidi ya Real Madrid kuiondoa Barca katika kombe tangu 2008.Mchezo wa marudiano utapigwa Nou Camp Jumatano, 11 Januari.
Thus articles Copa del Rey: Athletic Bilbao 2-1 Barcelona: Barca yachapwa na wachezaji tisa
that is all articles Copa del Rey: Athletic Bilbao 2-1 Barcelona: Barca yachapwa na wachezaji tisa This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article Copa del Rey: Athletic Bilbao 2-1 Barcelona: Barca yachapwa na wachezaji tisa the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2017/01/copa-del-rey-athletic-bilbao-2-1.html
0 Response to "Copa del Rey: Athletic Bilbao 2-1 Barcelona: Barca yachapwa na wachezaji tisa"
Post a Comment