Title : FIFA News: Cristiano Ronaldo ambwaga tena Lionel Messi
link : FIFA News: Cristiano Ronaldo ambwaga tena Lionel Messi
FIFA News: Cristiano Ronaldo ambwaga tena Lionel Messi
Cristiano Ronaldo ametajwa kuwa Mchezaji Bora wa Dunia wa Mwaka maarufu kama Best Fifa Football Awards katika tuzo zilizofanyika mjini Zurich, Uswisi.
Fowadi wa Real Madrid na Ureno Ronaldo, 31, aliwabwaga wapinzani wake nyota wa Barcelona na Argentina Lionel Messi na mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ufaransa Antoine Griezmann.
Ronaldo pia alitwaa tuzo ya Ballon d'Or mwezi Disemba, ambazo tuzo zote zikitokana na mchango mkubwa katika kutwaa Champions League akiwa na Real na Euro 2016 akiwa na Ureno.
Carli Lloyd wa United States alitajwa kuwa Mchezaji Bora wa kike wakati meneja wa Leicester City Claudio Ranieri akiwa Meneja Bora wa mwaka, huku boss wa zamani wa Ujerumani Silvia Neid akitwaa tuzo hiyo kwa upande wa wanawake, na mchezaji wa Penang Mohd Faiz Subri akipata tuzo ya Bao Bora 2016.
Mwaka 2016 ulikuwa bora kwa Ronaldo.
Pamoja na kufunga penalti ya ushindi kwenye Champions League, kuifungia Real hat-trick kwenye fainali ya Club World Cup, kuiongoza Ureno kutwaa Euro 2016 na kunyakua tuzo ya nne ya Ballon d'Or, sasa amefanya kitu ambacho Messi hajakifanya - heshima ya kutajwa kuwa Mchezaji Bora wa kiume wa Fifa.
Fowadi wa zamani wa Manchester United amejikusanyia tuzo, kufuatia mwaka alioendelea kuwa na takwwimu nzuri. Hizi baadhi yazo:
- Mechi 44, mabao 42, assist 14.
- Uwiano wa dakika tatu kwa bao (83.68) ya yeyote anayefunga mabao 10 katika Ligi Kuu r bora barani Europe mwaka 2016, nyuma ya Luis Suarez (82.57) na Radamel Falcao (59.6).
- Alimaliza kinara wa mabao kwenye Champions League msimu wa 2015-16 akiwa na mabao 16, saba zaidi ya mtu wa nafasi ya pili Robert Lewandowski.
Matokeo
Cristiano Ronaldo: 34.54% ya kura zote
Lionel Messi: 26.42%
Antoine Griezmann: 7.53%
Fifpro World XI
Wachezaji wa Barcelona na Real Madrid wametawala kwenye timu ya Fifa na FIFPro.
Thus articles FIFA News: Cristiano Ronaldo ambwaga tena Lionel Messi
that is all articles FIFA News: Cristiano Ronaldo ambwaga tena Lionel Messi This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article FIFA News: Cristiano Ronaldo ambwaga tena Lionel Messi the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2017/01/fifa-news-cristiano-ronaldo-ambwaga.html
0 Response to "FIFA News: Cristiano Ronaldo ambwaga tena Lionel Messi"
Post a Comment