Title : Tetesi za usajili: Manchester United yamuweka sokoni Schneiderlin, Guardiola aichokonoa Atletico Madrid kwa Lucas Hernandez, Spurs yamuwekea mwichi Alli, Batshuayi kuondoka Chelsea, Sunderland yambania Defoe
link : Tetesi za usajili: Manchester United yamuweka sokoni Schneiderlin, Guardiola aichokonoa Atletico Madrid kwa Lucas Hernandez, Spurs yamuwekea mwichi Alli, Batshuayi kuondoka Chelsea, Sunderland yambania Defoe
Tetesi za usajili: Manchester United yamuweka sokoni Schneiderlin, Guardiola aichokonoa Atletico Madrid kwa Lucas Hernandez, Spurs yamuwekea mwichi Alli, Batshuayi kuondoka Chelsea, Sunderland yambania Defoe
Manchester United inataka zaidi ya paundi 20m kwa kiungo Morgan Schneiderlin, 27, ambaye amekuwa akiwindwa na West Brom na Everton. (Manchester Evening News)
Miamba ya soka la Ufaransa Marseille pia imejiunga katika mbio za kuinasa saini ya Schneiderlin na inaweza kufikia matakwa ya United. (Sun)
Kiungo wa United Michael Carrick, 35, angali anasubiri kupewa ofa ya mkataba mpya, ambapo mkataba wa sasa ukitarajia kuchina majira ya joto, na sasa yuko huru kufanya mazungumzo na klabu yoyote. (Sun)
Boss wa Manchester City Pep Guardiola atasubiri hadi majira ya joto ili kufanya usajili wa mlinzi wa Atletico Madrid Lucas Hernandez, 20. Mfaransa huyo ana thamani ya paundi 20m kwa mujibu wa klabu hiyo ya La Liga. (Independent)
Guardiola anasema itaichukua klabu hiyo miaka 10 kuwafikia majirani zao United kwa ubora katika soka la Ulaya. (Daily Mirror)
Tottenham haitomuuza kiungo Dele Alli, 20, kwa bei yoyote baada ya kuzagaa kwa taarifa kuwa Real Madrid inataka kulipa paundi 50m. (Sky Sports)
Manchester United na Manchester City zinawawinda mlinzi Jordan Bedeau, 17, na fowadi Callum Styles, 16, ambao wanacheza kwenye League One katika timu ya Bury ambapo wamekuwa katika kikosi cha kwanza. (ESPN)
City pia inavutiwa na kiungo wa Sevilla Steven N'Zonzi, 28, na wapo tayari kutoa paundi 25m ili awe mbadala wa majeruhi Ilkay Gundogan. (Sun)
Miamba ya Ligue 1 Lille wanataka kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi, 23, ambaye amecheza mara 11 pekee tangu alipojiunga na Blues kwa paundi 33m. (Daily Mirror)
Boss wa Chelsea Antonio Conte amemfanya kiungo wa West Ham Michail Antonio, 26, miongoni mwa machaguo yake anayoyahitaji. (Sun)
Kiungo wa Blues Jon Mikel Obi, 29, amepokea ofa kutoka klabu nne za Chinese Super League - mkataba wa kiungo huyo wa Nigeria katika dimba la Stamford Bridge unachina majira ya joto. (Daily Mirror)
Mlinzi wa pembeni wa Napoli Faouzi Ghoulam, 25, amekataa ofa ya mkataba mpya akiwa na lengo la kujiunga na vinara wa Premier League Chelsea. (Evening Standard)
Sunderland imeikataa ofa ya West Ham kutaka kumsajili tena mshambuliaji Jermain Defoe, 34, kwa paundi 5m. (Mirror)
Mshambuliaji wa West Ham Simone Zaza, 25, ambaye ameshindwa kufunga tangu alipojiunga klabuni hapo kwa mkopo majira ya joto, atarejea Serie A katika sehemu ya msimu iliyobaki, kwa mujibu wa wakala wake. (Evening Standard)
The Hammers, Everton na Swansea zinapigana vikumbo kuiwania saini ya mshambuliaji wa RB Leipzig David Selke, 21, ambaye amefunga mabao 10 katika kuipandisha timu yake kwenye Bundesliga. (Daily Mail)
Watford imetoa ofa ya paundi 8m kwa mshambuliaji wa Brentford Scott Hogan, 24, ambaye amefunga mabao 14 kwenye mechi 25 za Championship msimu huu. (Guardian)
Liverpool imekataa ofa kutoka klabu tano zinazomhitaji kiungo Kevin Stewart, 23, kwa sababu boss Jurgen Klopp anamhitaji. (Liverpool Echo)
Everton itamsajili mlinzi wa Middlesbrough Ben Gibson, 23, kama watashindwa kumnasa windo la meneja Ronald Koeman Virgil van Dijk, 25, mwenye thamani ya paundi 50m katika kikosi cha Southampton. (Daily Mirror)
Mabingwa wa Premier League Leicester inataka kumsajili winga wa Norwich Robbie Brady, 24, mara tu watakapomuuza Bartosz Kapustka, 20, ambaye hajawahi kuichezea klabu hiyo. (Daily Mirror)
West Brom inataka kumsajili mshambuliaji wa Southampton Shane Long, 29, na mlinzi wa mlinzi wa Leeds Charlie Taylor, 23, mwezi huu. (Sun)
Aston Villa imetoa ofa ya paundi 3m kumsajili kiungo wa Nottingham Forest Henri Lansbury, 26, baada ya ofa ya paundi 2.5m kutoka kwa Derby kwa ajili ya mchezaji huyo kukataliwa. (Birmingham Mail)
Kiungo wa QPR Tjaronn Chery, 28, anakaribia kutua Chinese Super League kwenye klabu ya Guizhou Hengfeng Zhicheng kwa paundi 4m. (Sky Sports)
Birmingham imetoa ofa ya paundi 4m kwa winga wa Crystal Palace Bakary Sako, 28. Winga wa huyo wa Mali amecheza mara nne pekee katika kikosi cha Eagles msimu huu. (Daily Mail)
Boss wa Wolves Paul Lambert anataka kumsajili kiungo wa Blackburn Ben Marshall, 25, akiwahi kufanya kazi na mchezaji huyo Ewood Park. (Mirror)
Thus articles Tetesi za usajili: Manchester United yamuweka sokoni Schneiderlin, Guardiola aichokonoa Atletico Madrid kwa Lucas Hernandez, Spurs yamuwekea mwichi Alli, Batshuayi kuondoka Chelsea, Sunderland yambania Defoe
that is all articles Tetesi za usajili: Manchester United yamuweka sokoni Schneiderlin, Guardiola aichokonoa Atletico Madrid kwa Lucas Hernandez, Spurs yamuwekea mwichi Alli, Batshuayi kuondoka Chelsea, Sunderland yambania Defoe This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article Tetesi za usajili: Manchester United yamuweka sokoni Schneiderlin, Guardiola aichokonoa Atletico Madrid kwa Lucas Hernandez, Spurs yamuwekea mwichi Alli, Batshuayi kuondoka Chelsea, Sunderland yambania Defoe the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2017/01/tetesi-za-usajili-manchester-united.html
0 Response to "Tetesi za usajili: Manchester United yamuweka sokoni Schneiderlin, Guardiola aichokonoa Atletico Madrid kwa Lucas Hernandez, Spurs yamuwekea mwichi Alli, Batshuayi kuondoka Chelsea, Sunderland yambania Defoe"
Post a Comment