Title : League Cup: Manchester United v Southampton: Ni ama Mashetani au Watakatifu kwenye fainali ya kukata na shoka
link : League Cup: Manchester United v Southampton: Ni ama Mashetani au Watakatifu kwenye fainali ya kukata na shoka
League Cup: Manchester United v Southampton: Ni ama Mashetani au Watakatifu kwenye fainali ya kukata na shoka
MARTIN Caceres anaweza kucheza kwa mara ya kwanza kwa Southampton kwenye fainali ya EFL Cup dhidi ya Manchester United ambapo Saints wakitafuta taji lao la kwanza tangu 1976.
Caceres, 29, mlinzi wa zamani wa Barcelona na Juventus alijiunga na klabu hiyo wiki iliyopita na kumshawishi boss Claude Puel wakati wa mazoezi nchini Uhispania.
Nahodha wa United Wayne Rooney, ambaye amekuwa akihusishwa na kutaka kutimkia Uchina, atajumuishwa, alisema boss Jose Mourinho.
Mourinho anataka nyongeza ya mataji matatu ya League Cup aliyoshinda akiwa na Chelsea.
Ushindi katika mchezo wa Jumapili utakaopigwa Wembley utamfanya Mreno huyo kushinda taji kubwa katika msimu wake wa kwanza akiwa boss wa United.
"Jambo la muhimu ni klabu na hasa klabu ilishinda taji hili msimu uliopita," alisema, akirejelea mafanikio ya Red Devils kwenye FA Cup.
Taarifa za timu
Kiungo mshambuliaji wa United Henrikh Mkhitaryan ataukosa mchezo huu baada ya kuumia wakati wa mchezo wa Europa League ambao United walishinda bao 1-0 dhidi ya Saint-Etienne Jumatano iliyopita.
Kiungo Michael Carrick yuko fiti licha ya kuumia kifundo cha mguu Ufaransa, wakati maamuzi ya mwisho yatafanywa juu ya mlinzi Phil Jones, ambaye ana tatizo la mguu.
Southampton ina matumaini mchezaji Sofiane Boufal atarejea baada ya kuumia enka.
Charlie Austin, Virgil van Dijk, Jeremy Pied, Matt Targett na Alex McCarthy watakosekana kwa muda mrefu.
Uso-kwa-uso
- Hii ni mara ya pili timu hizi kukutana kwenye fainali ya mashindano haya, wakicheza nyingine mwaka 1976 kwenye fainali ya FA Cup. Southampton, wakati huo daraja la pili, waliishinda United kwa bao 1-0 shukrani kwa bao la Bobby Stokes. Inasalia kuwa muda pekee kushinda taji katika historia ya soka la Uingereza.
- Southampton itakuwa timu ya tatu kucheza na United kwenye fainali zote za FA Cup na League Cup, ikifuatiwa na Aston Villa na Liverpool.
Manchester United
- Hii itakuwa fainali ya tisa kwa United kwenye League Cup. Wameshinda nne na kupoteza nne, lakini ushindi mara tatu kati ya hizo zimekuwa fainali tatu zilizopita (2006 v Wigan, 2009 v Spurs na 2010 v Aston Villa).
- Ni Liverpool pekee (12) imecheza fainali nyingi za League Cup zaidi ya United (tisa) na ni Arsenal pekee (tano) imepoteza fainali nyingi zaidi ya Red Devils.
- Jose Mourinho ametnga fainali ya League Cup mara tatu (akiwa meneja wa Chelsea mwaka 2005, 2007 na 2015), akishinda fainali zote. Ana uwino mzuri wa kushinda kwenye fainali za League Cup.
- Ni Brian Clough (nne) na Sir Alex Ferguson (nne) wameshinda League Cup mara nyingi zaidi ya Jose Mourinho (tatu).
- Mourinho hajapoteza fainali ya makombe ya ndani ya Uingereza katika maisha yake, pia alishinda FA Cup mwaka 2007.
- Zlatan Ibrahimovic amefunga mabao manne kwenye fainali nne za makombe ya ndani alizocheza akiwa na Paris St-Germain (ukiondoa Super Cups), akifunga mara mbili mwaka 2015 kwenye fainali Coupe de la Ligue dhidi ya Bastia, na mara mbili tena mwaka 2016 kwenye fainali ya Coupe de France dhidi ya Marseille.
Southampton
- Southampton ni timu ya pili kwenye historia ya League Cup kutinga fainali bila kuruhusu bao - Tottenham Hotspur ilifanya hivyo msimu wa 1981-82, lakini ilichapwa mabao 3-1 kwenye fainali na Liverpool.
- Claude Puel ametinga fainali za makombe ya ndani mara moja katika umeneja wake, akiiongoza Monaco kwenye fainali ya French League Cup mwaka 2001, ambako walichapwa mabao 2-1 dhidi ya Lyon.
Thus articles League Cup: Manchester United v Southampton: Ni ama Mashetani au Watakatifu kwenye fainali ya kukata na shoka
that is all articles League Cup: Manchester United v Southampton: Ni ama Mashetani au Watakatifu kwenye fainali ya kukata na shoka This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article League Cup: Manchester United v Southampton: Ni ama Mashetani au Watakatifu kwenye fainali ya kukata na shoka the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2017/02/league-cup-manchester-united-v.html
0 Response to "League Cup: Manchester United v Southampton: Ni ama Mashetani au Watakatifu kwenye fainali ya kukata na shoka"
Post a Comment