Title : Bundesliga: Bayern Munich 2-1 Bayer Leverkusen: Njia yasafika kwa Bavarian
link : Bundesliga: Bayern Munich 2-1 Bayer Leverkusen: Njia yasafika kwa Bavarian
Bundesliga: Bayern Munich 2-1 Bayer Leverkusen: Njia yasafika kwa Bavarian
Mats Hummels alifunga bao lake la kwanza la Bundesliga akiwa na Bayern Munich wakiichapa Bayer Leverkusen mabao 2-1 wakipaa kileleni mwa msimamo kwa pointi tatu juu ya RB Leipzig.
Thiago aliwafungia mabingwa hao bao la kuongoza baada ya Bernd Leno kuokoa shuti la Philipp Lahm.
Hakan Calhanoglu akasawazisha akimtungua Manuel Neuer kufuatia gongeana safi na Julian Brandt.
Lakini Hummels akafunga bao la kichwa akiunganisha kona ya Joshua Kimmich.
Bayern, ambayo inalisaka taji la tano mfululizo, ilipoteza mechi mbili zilizopita kwenye mashindano yote, na kushindwa kushinda kwenye mechi tatu, katika mwanzo wa Carlo Ancelotti.
Kwingineko, Borussia Dortmund iliporomoka hadi nafasi ya sita baada ya kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Eintracht Frankfurt, huku Haris Seferovic akifunga bao la ushindi baada ya Pierre-Emerick Aubameyang kusawazisha.
Timu ya nafasi ya tano Hoffenheim ilitoka sare ya bao 1-1 na Borussia Monchengladbach na kusalia timu isiyofungika - licha ya kushinda mara tano pekee katika mechi 12.
Kiungo wa zamani wa Arsenal Serge Gnabry aliendelea kuwa na msimu mzuri akifunga bao la kusawazisha Werder Bremen ikitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Hamburg.
Thus articles Bundesliga: Bayern Munich 2-1 Bayer Leverkusen: Njia yasafika kwa Bavarian
that is all articles Bundesliga: Bayern Munich 2-1 Bayer Leverkusen: Njia yasafika kwa Bavarian This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article Bundesliga: Bayern Munich 2-1 Bayer Leverkusen: Njia yasafika kwa Bavarian the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/11/bundesliga-bayern-munich-2-1-bayer.html
0 Response to "Bundesliga: Bayern Munich 2-1 Bayer Leverkusen: Njia yasafika kwa Bavarian"
Post a Comment