Title : EPL: Crystal Palace v Manchester City: Steve Mandanda nje wiki kadhaa, Bacary Sagna arejea
link : EPL: Crystal Palace v Manchester City: Steve Mandanda nje wiki kadhaa, Bacary Sagna arejea
EPL: Crystal Palace v Manchester City: Steve Mandanda nje wiki kadhaa, Bacary Sagna arejea
MLINDA mlango wa Crystal Palace Steve Mandanda atakosekana kwa wiki kadhaa kutokana na majeraha ya goti hivyo Wayne Hennessey atachukua nafasi yake Jumamosi dhidi ya Manchester City.
Joe Ledley na Lee Chung-yong wataangaliwa uimara wao, wakati Loic Remy na Pape Souare atasalia nje kwa muda mrefu.
Manchester City itamkrabisha mlinzi wa pembeni Bacary Sagna, ambaye amerejea karibuni kutoka kwenye majeraha.
Vincent Kompany atakuwepo, baada ya kujiondoa kwenye mechi za kimataifa.
Crystal Palace v Manchester City
Uso-kwa-uso
- Manchester City imeshinda mara 10 kati ya 11 dhidi ya Crystal Palace kwenye mashindano yote.
- Ushindi pekee katika mbio hizo kwa Palace ni mabao 2-1 kwenye Premier League katika mchezo uliopigwa Selhurst Park Aprili 2015.
- Palace imeshindwa kufunga bao kwenye mechi tano kati ya sita za Premier League dhidi ya City.
Crystal Palace
- Palace imecheza mechi 16 za Premier League bila clean sheet, safari ndefu sana kwa timu ya Ligi Kuu. Clean sheet yao ya mwisho kwenye Premier League ilikuwa dhidi ya Everton kwenye dimba la Selhurst Park 13 Aprili.
- Imepoteza mechi nne mfululizo kwenye ligi - licha ya kufunga mara mbili kwenye kila mechi kati ya mechi mbili za mwisho. Kichapo kitawakilisha mbio zao mbovu tangu kupoteza mechi tano mfululizo kuanzia Januari naaa Februari mwaka huu.
- Imevuna pointi 0.73 kwa mchezo mwaka 2016, wastani mbaya zaidi kwenye timu yoyote kwenye ligi nne kwenye soka la England.
- Kama mechi zingaliishia kipindi cha kwanza msimu huu, Palace ingekuwa mkiani mwa Premier League ikiwa na pointi sita.
- Connor Wickham amevunga mabao matatu ya Premier League dhidi ya Manchester City.
Manchester City
- City ina pointi 24, idadi ndogo kwa Pep Guardiola akiwa kama meneja baada ya mechi 11 msimu huu.
- Imeshindwa kuwa na clean sheet kwenye mechi 11 za ligi msimu huu.
- David Silva ameziona nyavu mara tatu kwenye mechi tatu za mwisho dhidi ya Crystal Palace.
- Sergio Aguero amefunga bao la ufunguzi kwenye mechi tano za Premier League msimu huu - zaidi ya mchezaji yeyote.
- Kevin de Bruyne ametoa assist sita msimu huu, zaidi ya mchezaji yeyote.
Thus articles EPL: Crystal Palace v Manchester City: Steve Mandanda nje wiki kadhaa, Bacary Sagna arejea
that is all articles EPL: Crystal Palace v Manchester City: Steve Mandanda nje wiki kadhaa, Bacary Sagna arejea This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article EPL: Crystal Palace v Manchester City: Steve Mandanda nje wiki kadhaa, Bacary Sagna arejea the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/11/epl-crystal-palace-v-manchester-city.html
0 Response to "EPL: Crystal Palace v Manchester City: Steve Mandanda nje wiki kadhaa, Bacary Sagna arejea"
Post a Comment