Title : League Cup: Liverpool 2-0 Leeds United: The Reds watinga nusu-fainali
link : League Cup: Liverpool 2-0 Leeds United: The Reds watinga nusu-fainali
League Cup: Liverpool 2-0 Leeds United: The Reds watinga nusu-fainali
KINDA Ben Woodburn amempiku Michael Owen na kuwa mfungaji kinda zaidi kuwahi kuifungia Liverpool baada ya the Reds kuichapa Leeds United mabao 2-0 kwenye robo-ainali ya EFL Cup uliopigwa Anfield.
Miamba hiyo ya Premier League ilipata bao la kwanza kupitia kwa Divock Origi ambaye aliihadaa safu ya ulinzi wa Leeds na kumtungua Trent Alexander-Arnold.
Wakajihakikishia nafasi kwenye nne bora baada ya mshambuliaji wa Wales U19 Woodburn, akiwa na umri wa miaka 17 na siku 45, kufunga bao la pili.
Liverpool iligonga mwamba kupitia kwa Georginio Wijnaldum kabla ya bao la kwanza huku naye winga wa Leeds Kemar Roofe akikosa bao dakika chache baada ya kuanza kipindi cha pili.
Liverpool itacheza nusu-fainali baada ya droo itakayofanywa baada ya mechi za Jumatano.
Katika mchezo mwingine wa robo-fainali Newcastle United ilikosa penalti tatu Hull City ikiichapa vinara hao wa Championship mabao 3-1 kwa penalti na kutinga nusu-fainali ya EFL Cup.
Kipa wa Hull Eldin Jakupovic aliokoa penalti mbili baada ya wenyeji kucheza dakika zote za nyongeza wakiwa 10 kufuatia Dieumerci Mbokani kutolewa.
Newcastle iliongoza baada ya muda nyongeza baada ya Mohamed Diame kufunga akiunganisha krosi ya Vurnon Anita.
Bao hilo lilidumu kwa dakika moja, Robert Snodgrass akasawazisha.
Thus articles League Cup: Liverpool 2-0 Leeds United: The Reds watinga nusu-fainali
that is all articles League Cup: Liverpool 2-0 Leeds United: The Reds watinga nusu-fainali This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article League Cup: Liverpool 2-0 Leeds United: The Reds watinga nusu-fainali the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/11/league-cup-liverpool-2-0-leeds-united.html
0 Response to "League Cup: Liverpool 2-0 Leeds United: The Reds watinga nusu-fainali"
Post a Comment