Sports News: Jurgen Klinsmann atimuliwa Marekani

Sports News: Jurgen Klinsmann atimuliwa Marekani - Hallo friend ALL NEW, In the article you read this time with the title Sports News: Jurgen Klinsmann atimuliwa Marekani, we have prepared well for this article you read and download the information therein. hopefully fill posts Article Culinary, Article Culture, Article Economy, Article Politics, Article Sports, Article The latest, Article Updated, we write can understand. Well, happy reading.

Title : Sports News: Jurgen Klinsmann atimuliwa Marekani
link : Sports News: Jurgen Klinsmann atimuliwa Marekani

Read also


Sports News: Jurgen Klinsmann atimuliwa Marekani

MCHEZAJI na boss wa zamani wa Ujerumani Jurgen Klinsmann, 52, amefutwa kazi ya kuifundisha timu ya taifa la Marekani.
Klinsmann, ambaye alishinda Kombe la Dunia akiwa mchezaji wa Ujerumani mwaka 1990, alipewa jukumu la kuifundisha Marekani mwaka 2011.
"Tungali na matumaini tuna wachezaji bora kutusaidia kufuzu Kombe la Dunia Urusi 2018," alisema rais wa chama cha soka Marekani Sunil Gulati.
"Lakini kiwango na muenendo wa timu hadi hatua hii unatushawishi kuwa tunahitaji kwenda uelekeo mwingine."
Klinsmann aliiongoza Marekani kutinga hatua ya 16 kwenye fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil baada ya kumaliza juu ya Ureno kwenye hatua ya makundi.
Hata hivyo, ilichapwa nyumbani na Mexico mabao 2-1 na mabao 4-0 ugenini na Costa Rica kwenye mechi mbili za awali kufuzu fainali za 2018.
Timu hiyo haina pointi na ipo mkiani katika kundi lenye nchi sita, chini ya Panama na Honduras, zikisalia mechi tano kuelekea kufuzu.
"Mechi nyingine ya kufuzu itakuwa baadaye mwezi Machi, tuna miezi kadhaa ya kujiandaa," aliongeza Gulati.
"Tunahitaji kujua njia bora mbele kuhakikisha safari ya mafanikio kufuzu mara ya nane mfululizo kwenye fainali za Kombe la Dunia."
Mshambuliaji wa zamani wa Tottenham Klinsmann alikuwa anahusishwa na kazi ya kuinoa timu ya taifa la England baada ya Sam Allardyce kuiacha kazi hiyo mapema mwezi Septemba.


Thus articles Sports News: Jurgen Klinsmann atimuliwa Marekani

that is all articles Sports News: Jurgen Klinsmann atimuliwa Marekani This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.

You are now reading the article Sports News: Jurgen Klinsmann atimuliwa Marekani the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/11/sports-news-jurgen-klinsmann-atimuliwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Sports News: Jurgen Klinsmann atimuliwa Marekani"

Post a Comment