UEFA: Arsenal 2-2 Paris St-Germain: Wenger akosa nafasi ya kuongoza Kundi A

UEFA: Arsenal 2-2 Paris St-Germain: Wenger akosa nafasi ya kuongoza Kundi A - Hallo friend ALL NEW, In the article you read this time with the title UEFA: Arsenal 2-2 Paris St-Germain: Wenger akosa nafasi ya kuongoza Kundi A, we have prepared well for this article you read and download the information therein. hopefully fill posts Article Culinary, Article Culture, Article Economy, Article Politics, Article Sports, Article The latest, Article Updated, we write can understand. Well, happy reading.

Title : UEFA: Arsenal 2-2 Paris St-Germain: Wenger akosa nafasi ya kuongoza Kundi A
link : UEFA: Arsenal 2-2 Paris St-Germain: Wenger akosa nafasi ya kuongoza Kundi A

Read also


UEFA: Arsenal 2-2 Paris St-Germain: Wenger akosa nafasi ya kuongoza Kundi A

Arsenal inakumbana na wakati mgumu kumaliza vinara kwenye kundi lao la Champions League baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Paris St-Germain kwenye dimba la Emirates.
The Gunners walikuwa wanatafuta ushindi ili kuwaweka kileleni mwa msimamo wa Kundi A baada ya miaka kadhaa ya kumaliza katika nafasi ya pili na kutolewa kwenye hatua ya mtoanokwa mara sita mfululizo.
Na ilionekana kuwa Arsenal walikuwa njiani licha ya kuwa nyuma dakika za mapema baada ya Edinson Cavani kufunga akimalizia krosi ya Blaise Matuidi.
Olivier Giroud akasawazisha kwa mkwaju wa penalti kabla ya mapumziko baada ya Grzegorz Krychowiak kumuangusha Alexis Sanchez. Na Arsenal ikawa mbele baada ya mpira wa marejeo kumgusa Marco Verratti kisha kujaa wavuni.
PSG walikuwa hatari zaidi na mpira wa kichwa uliopigwa na Lucas, ambao uliguswa na Alex Iwobi, ukawapa bao la ksawazisha zikisalia dakika 13.
Cavani akapoteza nafasi mbili za wazi na licha ya Arsenal na PSG kulingana pointi, mabingwa wa Ufaransa wananufaika na mabao ya ugenini huku ukisalia mchezo mmoja baada ya sare ya bao 1-1 baina yao mjini Paris.

Dondoo muhimu kuzifahamu

  • Hii ilikuwa mara ya kwanza kwenye mchezo wa Champions League kumalizika kwa mabao mengi zaidi ya mashuti yaliyolenga lango tangu Rangers vs Unirea Urziceni Oktoba 2009
  • Ni Lionel Messi (18) pekee amefunga mabao mengi zaidi ya Cavani (16) kwenye mashindano yote miongoni mwa wachezaji wa Ligi Kuu tano za Ulaya msimu huu
  • Mkwaju wa penalti ya Olivier Giroud ulikuwa shuti la kwanza kwa Arsenal la namna yoyote kwenye mechi
  • Giroud amefunga kwa mashuti yake tisa kati ya 11 yaliyolenga lango akiwa na Arsenal kwenye mashindano yote, akifunga mara mbili katika mashuti 22 kabla ya hapo
  • Arsenal haijapoteza mchezo katika mechi nne ilizokutana na PSG, tatu kati ya hizo zilimalizika kwa sare (W1)
  • PSG imeshindwa kuwa na clean sheet kwenye mechi zao 10 dhidi ya klabu za Uingereza
  • Arsenal imefunga mabao 14 kwenye hatua ya makundi - ni msimu wa 2010-11 (15) walifunga mabao mengi zaidi kwenye mechi 5 za awali hatua ya makundi Champions League

Kifuatacho?

Arsenal inarejea kwenye Premier League Jumapili itakapoikaribisha Bournemouth kwenye dimba la Emirates.


Thus articles UEFA: Arsenal 2-2 Paris St-Germain: Wenger akosa nafasi ya kuongoza Kundi A

that is all articles UEFA: Arsenal 2-2 Paris St-Germain: Wenger akosa nafasi ya kuongoza Kundi A This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.

You are now reading the article UEFA: Arsenal 2-2 Paris St-Germain: Wenger akosa nafasi ya kuongoza Kundi A the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/11/uefa-arsenal-2-2-paris-st-germain.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "UEFA: Arsenal 2-2 Paris St-Germain: Wenger akosa nafasi ya kuongoza Kundi A"

Post a Comment