Title : UEFA: Borussia Dprtimund 8-4 Legia Warsaw: Historia yawekwa UCL
link : UEFA: Borussia Dprtimund 8-4 Legia Warsaw: Historia yawekwa UCL
UEFA: Borussia Dprtimund 8-4 Legia Warsaw: Historia yawekwa UCL
Borussia Dortmund na Legia Warsaw zimeweka historia kwenye Champions League Jumanne - kwa mabao 12 kufungwa kwenye mchezo mmoja.
Vijana wa Thomas Tuchel waliwachapa wapinzani wao kutoka Poland mabao 8-4 kwenye mchezo wa kukumbukwa nchini Ujerumani.
Idadi hiyo inaipiku mabao 11 yaliyofungwa wakati Monaco ikiichapa Deportivo La Coruna mwaka 8-3 mwaka 2003.
Kulikuwa na mabao saba ndani ya dakika 22 za kipindi cha kwanza - na Legia ilimaliza kipindi cha kwanza ikifunga mabao manne kwenye Champions League lakini ilimaliza kwa kichapo.
Usiku wa kuvunja rekodi
- Ni mara ya kwanza kwenye historia ya Champions League wachezaji wanane kufunga kwenye mchezo mmoja.
- Dortmund inakuwa timu ya nne baada ya Liverpool, Monaco na Real Madrid kufunga mabao manane kwenye mchezo mmoja wa Champions League.
- Ulikuwa mchezo wa kwanza kwenye mashindano yoyote ya Europe kuwa na mabao 12 tangu Ajax ilipoichapa timu kutoka Luxembourg ya Red Boys Differdange mabao 14-0 kwenye mashindano yaliyojulikana zamani kama Uefa Cup 3 Oktoba 1984.
- Ni mchezo mmoja pekee kwenye historia ya European Cup na Champions League ilikuwa na mabao mengi - hiyo ilikuwa wakati klabu ya Uholanzi ya Feyenoord kuichapa KR ya Iceland mabao 12-2 Septemba 1969.
- Dortmund sasa imefunga mabao 14 dhidi ya Legia msimu huu wa Champions League - mengi zaidi dhidi ya mpinzani mmoja kwenye msimu wa Champions League.
- Shinji Kagawa - alipokuwa Manchester United - alifunga mabao mawili ndani ya sekunde 76, mabao ya haraka zaidi kwenye historia ya Champions League.
Thus articles UEFA: Borussia Dprtimund 8-4 Legia Warsaw: Historia yawekwa UCL
that is all articles UEFA: Borussia Dprtimund 8-4 Legia Warsaw: Historia yawekwa UCL This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article UEFA: Borussia Dprtimund 8-4 Legia Warsaw: Historia yawekwa UCL the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/11/uefa-borussia-dprtimund-8-4-legia.html
0 Response to "UEFA: Borussia Dprtimund 8-4 Legia Warsaw: Historia yawekwa UCL"
Post a Comment