Title : UEFA: Borussia Monchengladbach 1-1 Manchester City: Silva aipeleka City mtoano UCL
link : UEFA: Borussia Monchengladbach 1-1 Manchester City: Silva aipeleka City mtoano UCL
UEFA: Borussia Monchengladbach 1-1 Manchester City: Silva aipeleka City mtoano UCL
BAO la kusawazisha lililofungwa na David Silva liliihakikishia Manchester City nafasi ya kufuzu hatua ya mtoano wa Champions League kwa mara ya nne mfululizo kwa sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Borussia Monchengladbach.
City ilikuwa nyuma baada ya shuti kali la Raffael kumzidi ujanja Claudio Bravo na kujaa wavuni kuwaweka wenyeji mbele.
Lakini Silva alifanya kazi nzuri ya kumalizia krosi ya Kevin de Bruyne kuisawazishia City.
City iliimarika kipindi cha pili, ikisaidiwa na kutolewa kwa Lars Stindl kwa kadi mbili za manjano.
Hata hivyo, wageni walipunguzwa nao hadi kumi baada ya Fernandinho kuoneshwa pia kadi ya pili ya manjano akimvuta jezi Raffael kwenye nusu ya Monchengladbach.
Licha ya nafasi nyingi kwa pande zote mbili, mchezo huo ulimalizika kwa mabao hayo.
Lakini pointi, ukijumlisha na matokeo ya Celtic na Barcelona, yanawainua City ambao wanakamata nafasi ya pili kwenye Kundi C.
City hawatoweza kuwakamata mabingwa wa Uhispania, ambao wapo juu kwa pointi nne wakisaliwa na mchezo mmoja.
Kifuatacho?
Wanarudi kwenye Premier League ambapo City, ambao wako nyuma ya vinara Chelsea kwa pointi moja, watakuwa na safari kuifuata timu ya nafasi ya 12 kwenye msimamo Burnley Jumamosi.
Thus articles UEFA: Borussia Monchengladbach 1-1 Manchester City: Silva aipeleka City mtoano UCL
that is all articles UEFA: Borussia Monchengladbach 1-1 Manchester City: Silva aipeleka City mtoano UCL This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article UEFA: Borussia Monchengladbach 1-1 Manchester City: Silva aipeleka City mtoano UCL the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/11/uefa-borussia-monchengladbach-1-1.html
0 Response to "UEFA: Borussia Monchengladbach 1-1 Manchester City: Silva aipeleka City mtoano UCL"
Post a Comment