Title : EPL: Manchester City 1-3 Chelsea: Costa, Willian na Hazard wamshika pabaya Guardiola
link : EPL: Manchester City 1-3 Chelsea: Costa, Willian na Hazard wamshika pabaya Guardiola
EPL: Manchester City 1-3 Chelsea: Costa, Willian na Hazard wamshika pabaya Guardiola
USHINDI wa nane mfululizo wa Chelsea kwenye Premier League uliwahakikishia nafasi nzuri ya kutawala kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kufuatia kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 kwenye dimba la Etihad huku wenyeji wao Manchester City wakimaliza pungufu baada ya Sergio Aguero na Fernandinho kuoneshwa kadi nyekundu.
Vijana wa Antonio Conte walikuwa bora zaidi wakiwazidi uwezo City baada ya mapumziko kufuatia kuwa nyuma kwa bao la kujifunga la Gary Cahill alipokuwa anaokoa krosi ya Jesus Navas na kumchanganya kipa Thibaut Courtois.
Kevin de Bruyne akaikosesha City bao la wazi akipiga shuti lililogonga mwamba akiunganisha krosi ya Navas.
Chelsea wakasawazisha baada ya Diego Costa kumlamba chenga Nicolas Otamendi akafunga kisha wakatangulia mbele dakika 10 baadaye baada ya mchezaji wa akiba Willian kukimbia na mpira kisha kumtungua kipa wa City Claudio Bravo.
Eden Hazard akakamilisha ushindi kwa Chelsea akimzidi ujanja Aleksandar Kolarov kabla ya kufunga.
Ushindi wa nane mfululizo kwa Chelsea - dondoo
- Chelsea imeshinda mechi nane mfululizo kwenye Premier League kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2006-07, waliposhinda mechi tisa mfululizo wakati wa awamu ya kwanza ya utawala wa Jose Mourinho.
- Manchester City wamepoteza mchezo wa Premier League nyumbani ambao walianza kuongoza kwa mara ya kwanza tangu Aprili 2009 (1-3 v Fulham).
- Tangu kuanza kwa msimu wa 2013-14, mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa amefunga mabao 70 kwenye mechi 103 za ligi (Premier League na La Liga pamoja).
- City imeweka clean sheet kwenye mechi mbili kati ya 14 za Premier League games chini ya Pep Guardiola.
- Manchester City ilifanya mabadiliko sita kwenye kikosi chake cha kwanza kutoka kwenye mechi iliyopita ya Premier League (v Burnley) - imefanya jumla ya mabadiliko 46 ya kikosi cha kwanza msimu huu, zaidi ya timu yoyote.
Kifuatacho?
Manchester City watakuwa nyumbani dhidi ya Celtic kwenye Champions League Jumanne, wakifuatiwa na safari ya Leicester City kwenye Premier League 10 Disemba.
Mchezo ujao wa Chelsea watakuwa nyumbani dhidi ya West Bromwich Albion kwenye Premier League 11 Disemba.
Thus articles EPL: Manchester City 1-3 Chelsea: Costa, Willian na Hazard wamshika pabaya Guardiola
that is all articles EPL: Manchester City 1-3 Chelsea: Costa, Willian na Hazard wamshika pabaya Guardiola This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article EPL: Manchester City 1-3 Chelsea: Costa, Willian na Hazard wamshika pabaya Guardiola the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/epl-manchester-city-1-3-chelsea-costa.html
0 Response to "EPL: Manchester City 1-3 Chelsea: Costa, Willian na Hazard wamshika pabaya Guardiola"
Post a Comment