EPL: Premier League round-up: Jon Walters arejea kwenye mabao, Sanchez apiga hat-trick, Arsenal, Spurs zaua 5, Palace yaididimiza Southampton

EPL: Premier League round-up: Jon Walters arejea kwenye mabao, Sanchez apiga hat-trick, Arsenal, Spurs zaua 5, Palace yaididimiza Southampton - Hallo friend ALL NEW, In the article you read this time with the title EPL: Premier League round-up: Jon Walters arejea kwenye mabao, Sanchez apiga hat-trick, Arsenal, Spurs zaua 5, Palace yaididimiza Southampton, we have prepared well for this article you read and download the information therein. hopefully fill posts Article Culinary, Article Culture, Article Economy, Article Politics, Article Sports, Article The latest, Article Updated, we write can understand. Well, happy reading.

Title : EPL: Premier League round-up: Jon Walters arejea kwenye mabao, Sanchez apiga hat-trick, Arsenal, Spurs zaua 5, Palace yaididimiza Southampton
link : EPL: Premier League round-up: Jon Walters arejea kwenye mabao, Sanchez apiga hat-trick, Arsenal, Spurs zaua 5, Palace yaididimiza Southampton

Read also


EPL: Premier League round-up: Jon Walters arejea kwenye mabao, Sanchez apiga hat-trick, Arsenal, Spurs zaua 5, Palace yaididimiza Southampton

Burnley ilikumbana na kichapo cha tatu mfululizo kwenye Premier League msimu huu wakichapwa mabao 2-0 na Stoke City.
Mshambuliaji wa Jamhuri ya Ireland  Jon Walters aliunganisha krosi ya Mame Biram Diouf kufunga bao la kwanza tangu Machi kabla ya Marc Muniesa akafunga bao la pili akimalizia krosi ya Marko Arnautovic.
Mkiani mwa msimamo Crystal Palace waliondoa wasiwasi wa kushuka daraja baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Southampton kumaliza mbio za kuchapwa mara sita mfululizo.
Walinufaika na bao la kwanza baada ya Fraser Forster, mbele ya meneja mpya wa England Gareth Southgate, kuikosa pasi iliyorudishwa na Jose Fonte na kumuacha Benteke akishangilia siku yake ya kutimiza miaka 26.
James Tomkins akafunga bao la pili akiunganisha krosi ya Andros Townsend na Benteke akafunga tena.
Sunderland ilirekodi ushindi wao wa tatu msimu huu na kujiondoa eneo la kushuka daraja baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Leicester.
Walitangulia shukrani kwa bao la kujifunga la Robert Huth dakika ya 64 baada ya mlinzi huyo wa Leicester kutaka kuokoa mpira wa kichwa uliopigwa na Jan Kirchhoff huku Jermain Defoe akifunga bao la pili - likiwa bao lake la nane msimu huu.
Shinji Okazaki akaifungia Leicester bao la kufutia machozi dakika ya 80.
West Brom ikapanda juu ya timu ya nafasi ya sita Manchester United kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Watford.
Jonny Evans alifunga bao kuongoza akiunganisha kona ya Chris Brunt, ambaye baadaye naye free-kick yake ikambabatiza Juan Zuniga kwa bao la pili la Baggies.
Christian Kabasele akafunga bao la wageni, lakini kadi nyekundu ya Roberto Pereyra kwa mchezo usiokuwa wa kiungwana, ikamfanya Matt Phillips kumaliza udhia kwa bao la tatu kwa wenyeji.
Arsenal ikafanya kufuru baada ya kuwafukuzia Chelsea kileleni huku wakipitwa kwa pointi tatu kwa ushindi wa mabao 5-1.
Vijana wa Arsene Wenger walianza kufunga dakika ya 24 baada ya makosa ya Angelo Ogbonna kumfanya Alexis Sanchez kumtenegeneza Mesut Ozil, aliyefunga bao.
Fowadi wa Chile Sanchez akafunga bao la pili dakika ya 72 na akafunga tena dakika nane baadaye.
Mchezaji wa akiba wa West Ham Andy Carroll akafunga dakika ya 81, huku Alex Oxlade-Chamberlain akiifungia Arsenal bao la nne.
Sanchez akakamilisha idadi ya mabao 5 akifunga dakika ya 86 na kuwafanya Arsenal kufikisha mechi 13 bila kupoteza.
Harry Kane alifunga mara mbili na bao zuri la Son Heung-Min yaliwafanya Tottenham kushinda mabao 5-0 dhidi ya Swansea.
Fowadi wa England Kane alifunga kwa mkwaju wa penalti baada ya Kyle Naughton kumchezea vibaya Dele Alli.
Son akaifungia Tottenham bao la pili kabla ya mapumziko kabla ya Kane kufunga dakika nne baadaye baada ya kumda na Christian Eriksen kuifungia Tottenham mabao mawili ya mwisho dakika za 70 na 90 na kuiacha Swansea mkiani.


Thus articles EPL: Premier League round-up: Jon Walters arejea kwenye mabao, Sanchez apiga hat-trick, Arsenal, Spurs zaua 5, Palace yaididimiza Southampton

that is all articles EPL: Premier League round-up: Jon Walters arejea kwenye mabao, Sanchez apiga hat-trick, Arsenal, Spurs zaua 5, Palace yaididimiza Southampton This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.

You are now reading the article EPL: Premier League round-up: Jon Walters arejea kwenye mabao, Sanchez apiga hat-trick, Arsenal, Spurs zaua 5, Palace yaididimiza Southampton the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/epl-premier-league-round-up-jon-walters.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "EPL: Premier League round-up: Jon Walters arejea kwenye mabao, Sanchez apiga hat-trick, Arsenal, Spurs zaua 5, Palace yaididimiza Southampton"

Post a Comment