Title : EPL: Manchester City v Chelsea: Huku Sergio Aguero, kule Diego Costa vita ya uongozi Premier League
link : EPL: Manchester City v Chelsea: Huku Sergio Aguero, kule Diego Costa vita ya uongozi Premier League
EPL: Manchester City v Chelsea: Huku Sergio Aguero, kule Diego Costa vita ya uongozi Premier League
Manchester City itamuangalia Raheem Sterling, ambaye alilazimika kutolewa nje ya uwanja kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Burnley baada ya kupata majeraha madogo.
Kevin de Bruyne, John Stones, David Silva na Ilkay Gundogan wanaweza kuitwa kwenye kikosi cha kwanza.
Kocha mkuu wa Chelsea Antonio Conte anaweza kutobadilisha kikosi chake kwa mechi ya saba mfululizo kwenye Premier League.
John Terry anasalia nje wakati matatizo ya misuli kwa Mikel John Obi yataangaliwa upya.
Manchester City v Chelsea
Uso-kwa-uso
- Chelsea imepoteza mechi sita kati ya nane ilizoifuata Manchester City kwenye ligi na kombe, huku ushindi wao pekee ukija kwa bao la Branislav Ivanovic Februari 2014.
- City ilishinda mechi zote mbili za Premier League msimu uliopita kwa mabao 3-0. Chelsea iliichapa City mabao 5-1 kwenye FA Cup raundi ya tano Februari katika mchezo ambao wageni walichezesha kikosi dhaifu sana.
- Chelsea imeshinda mechi 11 ugenini dhidi ya Manchester City kwenye Premier League - jumla yao kubwa zaidi dhidi ya timu moja kwenye historia ya mashindano hayo.
Manchester City
- City imepoteza mara moja kati ya mechi 15 za ligi, ikishinda tisa na sare tano.
- Lakini imeweka clean sheet mbili katika mechi 16 za ligi.
- Sergio Aguero amefunga mara 16 kwenye mechi 18 za City msimu huu, yakiwemo 10 kwenye mechi 11 za ligi.
- Aguero alifunga mara nne kwenye mechi mbili dhidi ya Chelsea msimu uliopita, ikiwepo hat-trick katika dimba la Stamford Bridge.
- City imefanya mabadiliko mengi zaidi kwenye ligi - 40 kwenye kikosi cha kwanza msimu huu. Kinyume chake, mabadiliko saba ya Chelsea ni machache mno kwenye ligi
Chelsea
- Ushindi utaifanya Chelsea ikishinda mchezo wa nane mfululizo wa Premier League kwa mara ya kwanza tangu 2010 (mechi tatu za mwisho msimu wa 2009-10 na mechi saba za kwanza msimu wa 2010-11).
- Mbio hizo za ushindi zilimalizwa na kichapo cha bao 1-0 ugenini na Manchester City 25 Septemba 2010.
- Huu ni mwendo wao bora wa ushindi kwenye msimu mmoja tangu mechi tisa mfululizo msimu wa 2006-07.
- Diego Costa amehusika kwenye mabao 14 ya Premier League msimu huu (amefunga 10, ametoa assist manne) - mengi zaidi ya mchezaji yeyote.
- Nemanja Matic ametoa assist sita za Premier League msimu huu, ambazo ni moja zaidi ya alivyoweza kufanya kwenye misimu miwili iliyopita ikiwekwa pamoja.
- Chelsea ni timu pekee kwenye Premier League ambayo haijafunga au kufungwa kwa bao la kichwa msimu huu.
Thus articles EPL: Manchester City v Chelsea: Huku Sergio Aguero, kule Diego Costa vita ya uongozi Premier League
that is all articles EPL: Manchester City v Chelsea: Huku Sergio Aguero, kule Diego Costa vita ya uongozi Premier League This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article EPL: Manchester City v Chelsea: Huku Sergio Aguero, kule Diego Costa vita ya uongozi Premier League the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/epl-manchester-city-v-chelsea-huku.html
0 Response to "EPL: Manchester City v Chelsea: Huku Sergio Aguero, kule Diego Costa vita ya uongozi Premier League"
Post a Comment