Title : EPL News: Rungu la FA lawapitia Manchester City na Chelsea
link : EPL News: Rungu la FA lawapitia Manchester City na Chelsea
EPL News: Rungu la FA lawapitia Manchester City na Chelsea
KLABU za Manchester City na Chelsea zimeadhibiwa na FA kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wao wakati wa mchezo wa Premier League Jumamosi iliyopita.
Adhabu hiyo inafuata baada ya vurugu dakika ya 95 ya mchezo huo uliopigwa Etihad, ambapo Chelsea ilishinda kwa mabao 3-1.
City iliwapoteza fowadi Sergio Aguero na kiungo Fernandinho kwa kadi nyekundu, lakini kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas hatokumbana na adhabu yoyote.
Meneja wa City Pep Guardiola aliomba radhi kwa timu yake kujihusisha na kadhia hiyo.
Aguero, 28, amefungiwa mechi nne kwa kupata kadi nyekundu ya pili kwa vurugu uwanjani msimu huu, kufuatia rafu mbaya dhidi ya mlinzi wa Chelsea David Luiz.
Fernandinho alikwaruzana na Fabregas kwenye kadhia nyingine iliyotokana na rafu ya Aguero, na kiungo huyo wa Brazil atakosa mechi tatu.
Pia timu zote zimepewa hadi 8 Disemba kutoa mrejesho wa adhabu hizo.
Thus articles EPL News: Rungu la FA lawapitia Manchester City na Chelsea
that is all articles EPL News: Rungu la FA lawapitia Manchester City na Chelsea This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article EPL News: Rungu la FA lawapitia Manchester City na Chelsea the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/epl-news-rungu-la-fa-lawapitia.html
0 Response to "EPL News: Rungu la FA lawapitia Manchester City na Chelsea"
Post a Comment