Title : Tetesi za usajili: Paundi 60m kumpeleka Oscar Shanghai, Carlos Tevez kulipwa paundi 605,000-kwa-wiki, Edinson Cavani na Javier Pastore nao kutimkia Uchina
link : Tetesi za usajili: Paundi 60m kumpeleka Oscar Shanghai, Carlos Tevez kulipwa paundi 605,000-kwa-wiki, Edinson Cavani na Javier Pastore nao kutimkia Uchina
Tetesi za usajili: Paundi 60m kumpeleka Oscar Shanghai, Carlos Tevez kulipwa paundi 605,000-kwa-wiki, Edinson Cavani na Javier Pastore nao kutimkia Uchina
Soka la Uchina linajiandaa tena kushuhudia matumizi makubwa ya fedha kwa kumleta katika soka hilo nyota wa Brazil.
Mara hii ni matumizi ya paunsi 60m ambazo zinadaiwa kutaka kutumiwa na klabu ya Shanghai SIPG kumnasa kiungo wa Chelsea na Brazil Oscar.
- Klabu za Chinese Super League zinavutia wachezaji kutokana na kulipa vizuri
- Klabu hizi zipo tayari kutoa fedha zaidi ya thamani ya soko halisi
- Wanafurahia kulipa mishahara mikubwa
Oscar anatarajia kuwa mwanamichezo wa tatu anayelipwa zaidi kwenye michezo - akipokea paundi 400,000 kwa wiki - ingawa hadhi hiyo inaweza kudumu kwa muda mfupi huku taarifa zikidai kuwa majina mengine makubwa yanajiandaa kufuata fedha hizo mara tu baada ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili mwezi Januari.
Mbali na Oscar, nani anaweza kutua huko kabla ya msimu mpya wa 2017 Super League kuanza mwezi Machi?
Kuna uvumi mkubwa kuwa Shanghai Shenhua - inayofundishwa na boss wa zamani wa Sunderland Gus Poyet - inajiandaa kumsajili fowadi wa zamani wa Manchester United na Manchester City Carlos Tevez kutoka Boca Juniors katika dili linalodaiwa kuwa litamfanya mshambuliaji huyo wa Argentina kuvuna paundi 31.5m kwa mwaka - mshahara wa paundi 605,000-kwa-wiki.
Na France Football linaripoti kuwa mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani anaweza kujiunga na klabu iliyopanda daraja hivi karibuni ya Tianjin Quanjian - inayonolewa na mlinzi wa zamani wa Italia Fabio Cannavaro - kwa uhamisho wa euro 50m (paundi 41.79m) na mshahara wa paundi 16.7m kwa mwaka.
Pia inaarifiwa kuwa klabu hiyo inamhitaji kiungo wa Argentina Javier Pastore kutoka kwa mabingwa wa Ufaransa.
Thus articles Tetesi za usajili: Paundi 60m kumpeleka Oscar Shanghai, Carlos Tevez kulipwa paundi 605,000-kwa-wiki, Edinson Cavani na Javier Pastore nao kutimkia Uchina
that is all articles Tetesi za usajili: Paundi 60m kumpeleka Oscar Shanghai, Carlos Tevez kulipwa paundi 605,000-kwa-wiki, Edinson Cavani na Javier Pastore nao kutimkia Uchina This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article Tetesi za usajili: Paundi 60m kumpeleka Oscar Shanghai, Carlos Tevez kulipwa paundi 605,000-kwa-wiki, Edinson Cavani na Javier Pastore nao kutimkia Uchina the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/tetesi-za-usajili-paundi-60m-kumpeleka.html
0 Response to "Tetesi za usajili: Paundi 60m kumpeleka Oscar Shanghai, Carlos Tevez kulipwa paundi 605,000-kwa-wiki, Edinson Cavani na Javier Pastore nao kutimkia Uchina"
Post a Comment