Title : FA Cup: Manchester United 4-0 Reading: Rooney aweka rekodi mpya United
link : FA Cup: Manchester United 4-0 Reading: Rooney aweka rekodi mpya United
FA Cup: Manchester United 4-0 Reading: Rooney aweka rekodi mpya United
Wayne Rooney anakuwa mfungaji bora wa muda wote wa Manchester United mabingwa hao watetezi wakitinga raundi ya nne ya FA Cup kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Reading.
Rooney alifunga bao lake la 249 akiwa na United ndani ya dakika 10 kuifikia rekodi ya Sir Bobby Charlton iliyodumu kwa miaka 44, ambaye alikuwepo uwanjani kushuhudia tukio hilo.
Anthony Martial aliongeza bao la pili huku Marcus Rashford akifunga bao la tatu akiyatumia makosa ya mlinda mlango wa Reading Ali Al-Habsi chini ya mlinzi wa zamani wa United Jaap Stam,
Kwa United, huu ulikuwa ushindi wa nane mfululizo kwenye mashindano yote na ukiwa ni onyo kuelekea nusu-fainali ya EFL Cup Jumanne dhidi ya Hull.
Man Utd na Mourinho waendelea kushinda - dondoo muhimu kuzifahamu
- Rooney amefunga mabao matano kwenye mechi nne dhidi ya Reading.
- Manchester United imeshinda mechi nane mfululizo kwa mara ya kwanza tangu Septemba 2009.
- Hasa, huu ni mwendo mrefu wa ushindi kwa Mourinho kwa klabu ya Uingereza tangu Januari 2006 (mechi nane mfululizo akiwa na Chelsea).
- Martial amehusika katika mabao saba kwenye mechi saba za FA Cup (mabao matatu, assist nne).
- Mechi tatu za Reading ilizofungwa ugenini dhidi ya mpinzani wa Premier League kwenye FA Cup wamechapwa jijini Manchester (0-1 v City msimu wa 2010-11, 1-2 v United msimu wa 2012-13 na 0-4 v United msimu wa 2016-17).
- Al-Habsi ameruhusu mabao 17 kwenye mechi tano dhidi ya Manchester United katika dimba la Old Trafford.
- Reading ilipigiwa mashuti mengi zaidi (pamoja na yaliyozuwiwa) Jumamosi kuliko timu yoyote chini ya Stam msimu huu (mashuti 27).
Kifuatacho?
United watarejea dimbani katika dimba la Old Trafford Jumanne usiku kwa mchezo wa kwanza wa nusu-fainali ya EFL Cup dhidi ya Hull City, wakati mchezo ujao wa Reading watakuwa nyumbani kwenye Championship dhidi ya QPR Alhamisi.
Matokeo yote ya FA Cup raundi ya tatu:
Thus articles FA Cup: Manchester United 4-0 Reading: Rooney aweka rekodi mpya United
that is all articles FA Cup: Manchester United 4-0 Reading: Rooney aweka rekodi mpya United This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article FA Cup: Manchester United 4-0 Reading: Rooney aweka rekodi mpya United the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2017/01/fa-cup-manchester-united-4-0-reading.html
0 Response to "FA Cup: Manchester United 4-0 Reading: Rooney aweka rekodi mpya United"
Post a Comment