FA Cup: Blackburn Rovers 1-2 Manchester United: Zlatan Ibrahimovic aipeleka United mbele ya Chelsea

FA Cup: Blackburn Rovers 1-2 Manchester United: Zlatan Ibrahimovic aipeleka United mbele ya Chelsea - Hallo friend ALL NEW, In the article you read this time with the title FA Cup: Blackburn Rovers 1-2 Manchester United: Zlatan Ibrahimovic aipeleka United mbele ya Chelsea, we have prepared well for this article you read and download the information therein. hopefully fill posts Article Culinary, Article Culture, Article Economy, Article Politics, Article Sports, Article The latest, Article Updated, we write can understand. Well, happy reading.

Title : FA Cup: Blackburn Rovers 1-2 Manchester United: Zlatan Ibrahimovic aipeleka United mbele ya Chelsea
link : FA Cup: Blackburn Rovers 1-2 Manchester United: Zlatan Ibrahimovic aipeleka United mbele ya Chelsea

Read also


FA Cup: Blackburn Rovers 1-2 Manchester United: Zlatan Ibrahimovic aipeleka United mbele ya Chelsea

Zlatan Ibrahimovic alitokea kwenye benchi kufunga bao mabingwa watetezi Manchester United wakifanya kazi ya ziada kutoka nyuma na kuichapa Blackburn mabao 2-1 kwenye mchezo wa FA Cup raundi ya tano.

Mshambuliaji Ibrahimovic alipewa muda mwingi sana kwenye box na kuitendea haki pasi ya mchezaji-mwenza wa akiba Paul Pogba kufunga bao lililowapeleka United robo-fainali ambapo watacheza na vinara wa Premier League Chelsea.
Danny Graham aliwafungia wenyeji bao la kuongoza baada ya kazi nzuri ya Marvin Emnes, ambaye pia alimtia majaribuni Sergio Romero dakika za mwanzo wa mchezo.
Katika upand mwingine, kipa wa Rovers Jason Steele alifanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Ander Herrera, lakini Marcus Rashford aliwasawazishia United akimzunguka kipa na kumalizia pasi ya Henrikh Mkhitaryan.
Mshambuliaji wa Rovers Anthony Stokes alifunga bao lakini lilikataliwa akidaiwa alikwishaotea.
Katika mchezo mwingine wa FA Cup Fulham ilitupwa nje baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Tottenham.
Droo ya robo-fainali
Chelsea v Manchester United
Middlesbrough v Huddersfield/Manchester City
Tottenham v Millwall
Sutton/Arsenal v Lincoln

Kifuatacho?

Blackburn itasafiri kuifuata Burton Albion kwenye Championship Ijumaa ijayo, wakati Manchester United watakuwa na Saint-Etienne kwenye mchezo wa marudiano ya Europa League Jumatano.

Shujaa Ibrahimovic - dondoo

  • Zlatan Ibrahimovic sasa amefunga kwenye FA Cup, Coppa Italia, Copa del Rey na Coupe de France.
  • Mshambuliaji huyo wa Sweden sasa ni mfungaji-mwenza wa Manchester United kwenye mashindano yote tangu mwanzo wa msimu uliopita (mabao 24 - sawa na Anthony Martial), licha ya kujiunga klabuni hapo msimu huu.
  • Hakuna mchezaji wa Premier League aliyecheza mechi nyingi kwenye mashindano yote msimu huu zaidi ya Ibrahimovic na Nathan Redmond (36).
  • Assist zote tano za Paul Pogba kwa Manchester United msimu wa 2016-17 zimekwenda kwa Ibrahimovic.
  • Manchester United imesonga mbele katika mechi 11 za FA Cup dhidi ya timu za maraja ya chini.
  • Danny Graham alifunga bao lake la kwanza la FA Cup tangu Januari 2013, ambalo pia lilikuwa dhidi ya timu ya daraja la juu (Arsenal).
  • Assist nne kati ya tano za Henrikh Mkhitaryan kwa Manchester United zimepatikana kwenye mashindano ya kombe (tatu kwenye League Cup na moja kwenye FA Cup).
  • Marcus Rashford amefunga mabao manne kwenye mechi zake sita za FA Cup kwa Manchester United.
  • Blackburn imeweka clean sheet moja kwenye mechi 11 za nyumbani katika makombe ya ndani (FA Cup na League Cup).


Thus articles FA Cup: Blackburn Rovers 1-2 Manchester United: Zlatan Ibrahimovic aipeleka United mbele ya Chelsea

that is all articles FA Cup: Blackburn Rovers 1-2 Manchester United: Zlatan Ibrahimovic aipeleka United mbele ya Chelsea This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.

You are now reading the article FA Cup: Blackburn Rovers 1-2 Manchester United: Zlatan Ibrahimovic aipeleka United mbele ya Chelsea the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2017/02/fa-cup-blackburn-rovers-1-2-manchester.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "FA Cup: Blackburn Rovers 1-2 Manchester United: Zlatan Ibrahimovic aipeleka United mbele ya Chelsea"

Post a Comment