Title : Bundesliga: Bundesliga roundup: RB Leipzig yarejea kileleni, yaichapa Schalke; Borussia Dortmund yashinda 4-1
link : Bundesliga: Bundesliga roundup: RB Leipzig yarejea kileleni, yaichapa Schalke; Borussia Dortmund yashinda 4-1
Bundesliga: Bundesliga roundup: RB Leipzig yarejea kileleni, yaichapa Schalke; Borussia Dortmund yashinda 4-1
RB Leipzig iliipiku tena Bayern Munich kileleni mwa msimamo wa Bundesliga Jumamosi baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Schalke 04 kuwaacha mabingwa hao watetezi kwa pointi tatu.
Timu ya Carlo Ancelotti Bayern walirudi kileleni kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Mainz Ijumaa usiku, lakini Leipzig wakarejea kwenye nafasi yao saa 24 baadaye.
Bayern na Leipzig zinatarajia kukutana kwenye uwanja wa nyumbani wa Munich Allianz Arena Disemba 21.
Bao la kujifunga kipindi cha pili kutoka kwa mchezaji wa Schalke kutoka Bosnia Sead Kolasinac liliihakikishia ushindi Leipzig, ushindi wao wa 10 kwenye ligi, wakiendeleza rekodi yao ya kutofungwa mechi 13 za Bundesliga katika msimu wao wa kwanza.
Leipzig walipata bao la kuongoza mapema baada ya mlinda mlango wa Schalke Ralf Faehrmann kufutunguliwa kwa mkwaju wa penalti baada ya sekunde 19 baada ya mwamuzi kudai kuwa kipa huyo alimchezea vibaya mfungaji bora wa RB Timo Werner.
Katika mechi za mapema, Pierre-Emerick Aubameyang alifunga mara mbili Borussia Dortmund ikijiandaa kwa Champions League dhidi ya Real Madrid kwa mabao 4-1 dhidi ya Borussia Moenchengladbach.
Timu zote zimefuzu hatua ya 16, safari ya Bernabeu Jumatano itakuwa kuthibitisha nani atamaliza kinara wa Kundi F huku Dortmund ikifanya vizuri kwenye mchezo dhidi ya Moenchengladbach uliopigwa Signal Iduna Park.
Marco Reus alitoa assist tatu Dortmund ikitoka nyuma baada ya Gladbach kutangulia dakika ya sita kupitia kwa mshambuliaji wa Brazil Raffael.
Lukasz Piszczek akafunga kwa kichwa na Ousmane Dembele akafunga bao la pili.
Hertha Berlin wakapaa hadi nafasi ya tatu kwa ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Wolfsburg huku Salomon Kalou akifunga bao la ushindi kwa penalti dakika ya 91.
Hoffenheim, ambao sanjari na RB Leipzig ni timu pekee ambazo hazijafungwa kwenye Bundesliga, ipo nafasi ya nne baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Cologne.
Bayer Leverkusen, ambayo itawaalika vinara wa Kundi E Monaco Jumatano huku timu hizo zikifuzu hatua ya mtoano kwenye Champions League, ilitoka sare ya bao 1-1 na Freiburg.
Werder Bremen ilijinasua kutoka mkiani kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ingolstadt.
Thus articles Bundesliga: Bundesliga roundup: RB Leipzig yarejea kileleni, yaichapa Schalke; Borussia Dortmund yashinda 4-1
that is all articles Bundesliga: Bundesliga roundup: RB Leipzig yarejea kileleni, yaichapa Schalke; Borussia Dortmund yashinda 4-1 This time, hopefully can provide benefits to you all. Okay, see you in another article post.
You are now reading the article Bundesliga: Bundesliga roundup: RB Leipzig yarejea kileleni, yaichapa Schalke; Borussia Dortmund yashinda 4-1 the link address https://allnewsinformationtime.blogspot.com/2016/12/bundesliga-bundesliga-roundup-rb.html
0 Response to "Bundesliga: Bundesliga roundup: RB Leipzig yarejea kileleni, yaichapa Schalke; Borussia Dortmund yashinda 4-1"
Post a Comment